ASEC Mimosas
ASEC Mimosas (jina kamili ni Association Sportive des Employés de Commerce Mimosas) kwa maana halisi ni Chama cha Wafanyakazi wa Biashara wa Mimosas, ni klabu ya soka yenye makao yake katika mji wa Abidjan. Klabu hiyo pia inajulikana hasa katika mashindano ya kimataifa ya klabu kama ASEC Mimosas Abidjan au ASEC Abidjan.
Ilianzishwa mwaka 1948, na kuwa klabu yenye mafanikio zaidi katika soka wa Ivory Coast, baada ya kushinda Ligi Kuu ya Ivory Coast mara 24 na Ligi ya Mabingwa ya CAF mwaka 1998.[1]
Kituo cha kufundisha soka cha ASEC's Académie MimoSifcom kimezalisha idadi ya wachezaji maarufu zaidi wanaocheza na waliocheza katika ligi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na Bonaventure Kalou, Didier Zokora, Emmanuel Eboué, Bakari Koné, Gervinho, Salomon Kalou, Romaric, Boubacar Barry, Didier Ya Koné na, Kolo Toure, Yaya Toure na Odilon Kossounou, ambao wote wamecheza soka kimataifa.[2]
Marejeo
- ↑ "Asec Mimosas (Club sportif) – Abidjan.net Qui est qui ?". Abidjan.net. 21 Septemba 1960. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-06-12. Iliwekwa mnamo 2022-03-20.
{cite web}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "L'Express de Madagascar : Actualités en direct, politiques, économies, sports, cultures, madagascar, afrique, monde". Lexpressmada.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-12-15. Iliwekwa mnamo 2022-03-20.
Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu. Je, unajua kitu zaidi kuhusu ASEC Mimosas kama historia yake, uenezi au kanuni zake? Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |