Akida Korneli
Akida Korneli (kwa Kigiriki, Κορνήλιος, Kornelios) alikuwa akida wa kikosi cha Italia katika jeshi la Dola la Roma aliyefanya kazi huko Kaisarea Baharini (Palestina). Huko alivutiwa na dini ya Uyahudi hata akajitolea kujenga sinagogi, pamoja na kusali.
Wongofu wake na wa jamaa zake unasimuliwa mara tatu na Matendo ya Mitume kwa jinsi ulivyotiwa maanani na Luka mwinjili aliyetaka kueleza kwamba desturi ya kubatiza watu wa mataifa bila kudai kwanza watahiriwe ilianzisha na Mtume Petro kwa kuangazwa na Mungu (Mdo 10).
Suala hilo lilisumbua sana Kanisa la mwanzo hata baada ya Mtaguso wa Yerusalemu (49 BK) kupitisha desturi hiyo (Mdo 15).
Baada ya kuongoka, inasimuliwa kwamba alishuhudia Injili hadi Misia (leo nchini Uturuki) akateswa kwa ajili hiyo.
Habari nyingine zinasema alipata kuwa askofu na nyingine alifia dini, lakini hazisadikiki sana [1].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 20 Oktoba[2][3] lakini pia 13 Septemba au 2 Februari.
Tazama pia
- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
Viungo vya nje
- Saint Cornelius the Centurion at the Christian Iconography web site
- The Story of the Chapel of St. Cornelius the Centurion at Governor's Island, New York Harbor, Written for the Day of the Consecration, October 19, A.D. 1906. by Morgan Dix
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Akida Korneli kama habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |