Charles III wa Uingereza
Charles III (alizaliwa 14 Novemba 1948 kama Charles Philip Arthur George katika Buckingham Palace, London) ni mfalme wa Ufalme wa Muungano wa Britania na Eire ya Kaskazini tangu tarehe 8 Septemba 2022. Alipokea cheo hicho kutokana na kifo cha mama yake Malkia Elizabeth II[1].
Alirithi pia cheo cha ufalme wa nchi huru 14 zinazoitwa Commonwealth Realms:
- Antigua na Barbuda
- Australia
- Bahamas
- Belize
- Kanada
- Grenada
- Jamaika
- New Zealand
- Papua Guinea Mpya
- Saint Kitts na Nevis
- Saint Lucia
- Saint Vincent na Grenadini
- Visiwa vya Solomon
- Tuvalu
Yeye pia ni mkuu wa Jumuiya ya Madola, bwana wa maeneo yaliyopo chini ya Taji la Uingereza na mkuu wa kidunia wa Kanisa Anglikana nchini Uingereza.
Marejeo
- ↑ Prince Charles is king after death of mother, Queen Elizabeth II tovuti ya Guardian (UK) tarehe 0.09.2022
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Charles III wa Uingereza kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |