Daa-mguufarasi
Daa-mguufarasi
|
![Daa-mguufarasi wawili (Phoronis ijimai)](//upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/3/37/Phoronis_ijimai_130771917.jpg/250px-Phoronis_ijimai_130771917.jpg)
Daa-mguufarasi wawili (Phoronis ijimai)
|
Uainishaji wa kisayansi
|
Himaya:
|
Animalia
|
Nusuhimaya:
|
Eumetazoa
|
Faila ya juu:
|
Lophotrochozoa
|
Faila:
|
Phoronida Hatschek, 1888
|
Familia:
|
Phoronidae Hatschek, 1888
|
|
Ngazi za chini
|
Jenasi 2, spishi 13:
- Phoronis Wright, 1856
- P. australis Haswell, 1883
- P. embryolabi Temereva & Chichvarkhin, 2017
- P. emigi Hirose et al., 2014
- P. hippocrepia Wright, 1856
- P. ijimai Oka, 1897
- P. muelleri Selys-Longchamps, 1903
- P. ovalis Wright, 1856
- P. pallida Schneider, 1862
- P. psammophila Cori, 1889
- P. savinkini Temereva & Nekhlyudov, 2018
- Phoronopsis Gilchrist, 1907
- P. albomaculata Gilchrist, 1907
- P. californica Hilton, 1930
- P. harmeri Pixell, 1912
|
Daa-mguufarasi (kutoka kwa Kiing. horseshoe worm) ni wanyama wadogo wa bahari wa faila Phoronida. Faila hiyo ina familia moja tu na spishi 13. Wanyama hao wanafanana na daa wanaobeba taji ya minyiri kwa umbo la nusuduara au kwato ya farasi au kiatu chake. Hutokea katika bahari zote, isipokuwa Bahari ya Antaktiki ambapo hawajavumbuliwa. Kwa kawaida huishi katika neli ndani ya mashapo ya sakafu ya bahari kwa kina cha m 0-400.