Dieudonné Nzapalainga
Dieudonné Nzapalainga, C.S.Sp. (alizaliwa 14 Machi 1967) ni kiongozi wa Kanisa Katoliki kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati ambaye amekuwa Askofu Mkuu wa Bangui tangu 2012, ambapo alihudumu kama msimamizi wa kitume kutoka 2009 hadi 2012. Amekuwa rais wa Baraza la Maaskofu wa Kikatoliki wa Afrika ya Kati tangu 2013. Yeye ni mwanachama wa Waspiritani.
Papa Fransisko alipomteua kuwa kardinali mwaka 2016, alikua kardinali wa kwanza kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR), mwanachama mdogo zaidi wa Baraza la Makardinali, na wa kwanza kuzaliwa baada ya Mtaguso wa Pili wa Vatikano.[1]
Marejeo
- ↑ Chareton, Agnès (8 Juni 2021). "Centrafrique : Dieudonné Nzapalainga, le courage d'un cardinal". Le Pèlerin (kwa Kifaransa). Iliwekwa mnamo 24 Januari 2024.
{cite news}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
![]() |
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |