Efrem wa Syria

Picha takatifu ya Mt. Ephrem.
Picha takatifu ya Mt. Efrem iliyochorwa huko Meryemana Kilesesi, Diyarbakir, Uturuki.
Kanisa la Mt. Yakobo wa Nisibi, ambapo Efrem alikuwa akitoa huduma.

Efrem wa Siria (kwa Kiaramu: ܐܦܪܝܡ ܣܘܪܝܝܐ, Aphrêm Sûryāyâ; kwa Kiarabu أفرام السرياني; kwa Kigiriki: Ἐφραίμ ὁ Σῦρος, Ephraim Syros; kwa Kilatini: Ephraem Syrus; Nisibi, leo Nusaybin nchini Uturuki, 306 hivi - Edesa, leo Urfa, nchini Uturuki, 9 Juni 373), alikuwa mtawa na shemasi, mwanateolojia na mwanashairi pamoja.

Ni maarufu hasa kwa tenzi zake nyingi ajabu kwa lugha ya Kiaramu ambazo zinatumika hadi leo katika liturujia na kutokeza imani kwa namna bora.

Ndiye mwakilishi muhimu zaidi wa Ukristo wa Kisiria.

Kisha kufa akaheshimiwa na Waorthodoksi wa Mashariki, Waorthodoksi na Wakatoliki kama mtakatifu na babu wa Kanisa.

Papa Benedikto XV tarehe 5 Oktoba 1920 alimuongezea sifa ya mwalimu wa Kanisa.

Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe ya kifo chake[1].

Maisha

Efrem alizaliwa katika familia ya Kikristo mwaka 306 hivi huko Nisibi, leo Uturuki kusini mashariki, mipakani kwa Siria), akabatizwa alipokuwa na umri wa miaka 18.

Hakuoa, ingawa hakuna hakika kama mtindo wake wa maisha unaweza ukaitwa umonaki.

Kisha kulelewa na Yakobo, askofu wa Nisibi (303-338), alianzisha naye chuo cha teolojia katika mji huo.

Kwa muda mrefu na kwa bidii nyingi alifanya kazi ya ushemasi akihubiri na kufundisha teolojia na maisha ya Kiroho kwa wamonaki na walei wa huko hadi mwaka 363, ambapo Wakristo walifukuzwa na Waajemi kutoka mji huo.

Hapo naye pia akahamia Edesa, leo nchini Uturuki, alikoendelea kuhubiri hadi alipofariki tarehe 9 Juni 373 kutokana na maradhi aliyoambukizwa wakati wa kuwahudumia wagonjwa.

Alitetea imani sahihi dhidi ya uzushi wa mazingira yake (Uorigene, Uario na Gnosis) na kufanya umisionari kati ya wasio Wakristo.

Teolojia yake

Maandishi yake yanatokeza kuliko mengine yote Ukristo ulivyo kadiri ya mapokeo ya Kisemiti, yaliyo jirani na asili yake Kiyahudi kuliko yale ya Kigiriki na ya Kilatini yaliyotokea katika Dola la Roma. Pamoja na hayo, Efrem aliwahi kutengeneza mazingira na kwa namna fulani hata misamiati ya mafundisho rasmi juu ya Kristo yatakayotolewa na mitaguso mikuu ya karne V.

Mbali ya vitabu vya kupinga uzushi na vya kufafanua Biblia, vingine vyote vinafuata ushairi, na hata hotuba zake zilikuwa na mtindo huo. Ni kati ya watu waliotunga mashairi mengi zaidi katika historia ya fasihi. Inakadiriwa aliandika mistari milioni tatu kwa heshima ya Bikira Maria tu katika miaka 360-370. Ni kati ya waenezaji wakuu wa heshima hiyo, akisisitiza kwamba, kama vile hakuna ukombozi bila Yesu, vilevile hakuna umwilisho wake bila Maria. Fumbo hilo lilizidisha hadhi ya wanawake, ambao Efrem anawazungumzia daima kwa heshima ya dhati.

Ili kuelewa mafundisho yake, ni lazima kuzingatia daima kwamba alifanya teolojia kwa ushairi: huo ulimwezesha kuchimba mafumbo kwa njia ya mifano inayopingana ili kusisitiza maajabu yaliyofanywa na Mungu.

Kwa mfano, katika utenzi kuhusu Kuzaliwa kwa Kristo aliandika: “Bwana alimuingia Maria akawa mtumishi; Neno alimuingia akawa mkimya ndani ya Maria; ngurumo ilimuingia na sauti yake ikawa tulivu; Mchungaji alimuingia akawa Mwanakondoo ndani ya Maria akatoka akilia. Wewe uliyepanga yote, tumbo la Mama yako liligeuza utaratibu wa mambo. Yeye alimuingia tajiri, akatoka fukara: Aliye Juu alimuingia akatoka duni. Aliye uangavu alimuingia na kuvaa, akatoka ana sura nyonge… Yeye anayelisha wote aliingia akasikia njaa. Yeye anayenywesha wote aliingia akasikia kiu. Yeye anayepamba vyote alimtoka Maria akiwa uchi na tupu”.

Teolojia yake inakuwa liturujia, muziki: kweli alikuwa mtunzi mahiri akiunganisha kutafakari juu ya imani na kuimba sifa za Mungu. Ni katika hali hiyo kwamba ukweli unang’aa katika mafundisho yake kwa watu yaliyo rahisi kukaririwa na kuimbwa. Ndiyo mbinu ya kufana aliyotumia katika sikukuu ili kueneza imani ya Kanisa.

Ni mwanateolojia ambaye, juu ya msingi wa Biblia, anafikiri kishairi fumbo la ukombozi wa binadamu ulioletwa na Kristo, Neno wa Mungu aliyefanyika mtu.

Efrem alitumia pia mifano mingi ya viumbe mbalimbali, kwa kuwa kwake vyote vinashikamana, na ulimwengu ulioumbwa na Mungu ni kitabu cha kusomwa pamoja na Biblia.

Kwa ubora wa mashairi yake kuhusu imani kwa jumla ameitwa “kinubi cha Roho Mtakatifu”.

Sala yake

Mwokozi wetu, msalaba wako ulikomesha uhai wa mwili. Utujalie tusulubishe kiroho nafsi yetu. Ufufuko wako, Yesu, ukuze utu wa kiroho ndani mwetu… Umbile duni la mwili wetu linatuelekeza kufa. Mimina juu yetu upendo wako wa Kimungu, ufute moyoni mwetu matokeo ya sisi kuelekea kifo.

Tazama pia

Maandishi

a) Mfululizo « Sources Chrétiennes » (kwa Kifaransa)

  • ÉPHREM DE NISIBE, Commentaire de l’évangile concordant ou Diatessaron, introduction, traduction et notes par L. Leloir, Cerf, Paris 1966 (Sources Chrétiennes 121).
  • ÉPHREM DE NISIBE, Hymnes sur le Paradis, traduction par R. Lavenant, introduction et notes par F. Graffin, Cerf, Paris 1968 (Sources Chrétiennes 137).
  • ÉPHREM DE NISIBE, Hymnes sur la nativité, introduction par F. Graffin, traduction et notes par F. Cassingena–Trévedy, Cerf, Paris 2001 (Sources Chrétiennes 459).
  • ÉPHREM DE NISIBE, Hymnes Pascales, introduction, traduction et notes par F. Cassingena–Trévedy, Cerf, Paris 2006 (Sources Chrétiennes 502).

b) Mfululizo « Corpus Scriptorum Christianorum Orientalium » (Katika lugha asili na kwa Kijerumani, isipokuwa kitabu cha kwanza ambacho ni tafsiri ya Kilatini)

  • SAINT’ÉPHRAEM, Commentaire de l’Évangile concordant. Version ármenienne, traduite en latin par L. Leloir, Sécretariat du CorpusSCO, Louvain 1964 (Corpus Scriptorum Christianorum Orientalium 145).
  • DES HEILIGEN EPHRAEM DES SYRERS, Hymnen contra Haereses, Herausgegeben und Übersetzt von E. Beck, Sécretariat du CorpusSCO, Louvain 1957 (Corpus Scriptorum Christianorum Orientalium 169-170) .
  • DES HEILIGEN EPHRAEM DES SYRERS, Hymnen de Paradiso und contra Julianum, Herausgegeben und Übersetzt von E. Beck, Sécretariat du CorpusSCO, Louvain 1957 (Corpus Scriptorum Christianorum Orientalium 174-175).
  • DES HEILIGEN EPHRAEM DES SYRERS, Hymnen de Nativitate (Épiphania), Herausgegeben und Übersetzt von E. Beck, Sécretariat du CorpusSCO, Louvain 1959 (Corpus Scriptorum Christianorum Orientalium 186-187).
  • DES HEILIGEN EPHRAEM DES SYRERS, Hymnen de Ecclesia, Herausgegeben und Übersetzt von E. Beck, Sécretariat du CorpusSCO, Louvain 1960 (Corpus Scriptorum Christianorum Orientalium 198-199).
  • DES HEILIGEN EPHRAEM DES SYRERS, Sermones de Fide, Herausgegeben und Übersetzt von E. Beck, Sécretariat du CorpusSCO, Louvain 1961 (Corpus Scriptorum Christianorum Orientalium 212-213).
  • DES HEILIGEN EPHRAEM DES SYRERS, Carmina Nisibena. I, Herausgegeben und Übersetzt von E. Beck Sécretariat du CorpusSCO, Louvain 1961 (Corpus Scriptorum Christianorum Orientalium 218-219).
  • DES HEILIGEN EPHRAEM DES SYRERS, Hymnen de Verginitate, Herausgegeben und Übersetzt von E. Beck, Sécretariat du CorpusSCO, Louvain 1962 (Corpus Scriptorum Christianorum Orientalium 223-224).
  • DES HEILIGEN EPHRAEM DES SYRERS, Carmina Nisibena. II, Herausgegeben und Übersetzt von E. Beck, Sécretariat du CorpusSCO, Louvain 1963 (Corpus Scriptorum Christianorum Orientalium 240-241).
  • DES HEILIGEN EPHRAEM DES SYRERS, Hymnen de Ieiunio, Herausgegeben und Übersetzt von E. Beck, Sécretariat du CorpusSCO, Louvain 1964 (Corpus Scriptorum Christianorum Orientalium 246-247).
  • DES HEILIGEN EPHRAEM DES SYRERS, Paschahymnen (de azimis, de crucifixione, de resurrectione), Herausgegeben und Übersetzt von E. Beck, Sécretariat du CorpusSCO, Louvain 1964 (Corpus Scriptorum Christianorum Orientalium 248-249).
  • DES HEILIGEN EPHRAEM DES SYRERS, Hymnen de Fide, Herausgegeben und Übersetzt von E. Beck, Sécretariat du CorpusSCO, Louvain 1965 (Texte) 1967 (Version) (Corpus Scriptorum Christianorum Orientalium 154-155).
  • DES HEILIGEN EPHRAEM DES SYRERS, Sermo de Domino Nostro, Herausgegeben und Übersetzt von E. Beck, Sécretariat du CorpusSCO, Louvain 1966 (Corpus Scriptorum Christianorum Orientalium 269-270).
  • DES HEILIGEN EPHRAEM DES SYRERS, Sermones. I, Herausgegeben und Übersetzt von E. Beck Sécretariat du CorpusSCO, Louvain 1970 (Corpus Scriptorum Christianorum Orientalium 305-306).
  • DES HEILIGEN EPHRAEM DES SYRERS, Sermones. II, Herausgegeben und Übersetzt von E. Beck, Sécretariat du CorpusSCO, Louvain 1970 (Corpus Scriptorum Christianorum Orientalium 311-312).
  • DES HEILIGEN EPHRAEM DES SYRERS, Sermones. III, Herausgegeben und Übersetzt von E. Beck, Sécretariat du CorpusSCO, Louvain 1972 (Corpus Scriptorum Christianorum Orientalium 320-321).
  • DES HEILIGEN EPHRAEM DES SYRERS, Hymnen auf Abraham Kydunaya und Julianos Saba, Herausgegeben und Übersetzt von E. Beck, Sécretariat du CorpusSCO, Louvain 1972 (Corpus Scriptorum Christianorum Orientalium 322-323).
  • DES HEILIGEN EPHRAEM DES SYRERS, Sermones. IV, Herausgegeben und Übersetzt von E. Beck, Sécretariat du CorpusSCO, Louvain 1973 (Corpus Scriptorum Christianorum Orientalium 334-335)
  • EPHRAEM SYRUS, Nachträge, Herausgegeben und Übersetzt von E. Beck, Sécretariat du CorpusSCO, Louvain 1975 (Corpus Scriptorum Christianorum Orientalium 363-364).
  • EPHRAEM SYRUS, Sermones in Hebdomadam Sanctam, Herausgegeben und Übersetzt von E. Beck, Sécretariat du CorpusSCO, Louvain 1979 (Corpus Scriptorum Christianorum Orientalium 412-413).

c) Tafsiri za Kiingereza

  • Sancti Patris Nostri Ephraem Syri opera omnia quae exstant (3 vol), by Peter Ambarach Rome, 1737–1743.
  • Ephrem the Syrian Hymns, introduced by John Meyendorff, translated by Kathleen E. McVey. (New York: Paulist Press, 1989) ISBN 0-8091-3093-9
  • St. Ephrem Hymns on Paradise, translated by Sebastian Brock (Crestwood, NY: St. Vladimir's Seminary Press, 1990). ISBN 0-88141-076-4
  • Saint Ephrem's Commentary on Tatian's Diatessaron: An English Translation of Chester Beatty Syriac MS 709 with Introduction and Notes, translated by Carmel McCarthy (Oxford: Oxford University Press, 1993).
  • St. Ephrem the Syrian Commentary on Genesis, Commentary on Exodus, Homily on our Lord, Letter to Publius, translated by Edward G. Mathews Jr., and Joseph P. Amar. Ed. by Kathleen McVey. (Washington, DC: Catholic University of America Press, 1994). ISBN 978-0-8132-1421-4
  • St. Ephrem the Syrian The Hymns on Faith, translated by Jeffrey Wickes. (Washington, DC: Catholic University of America Press, 2015). ISBN 978-0-8132-2735-1
  • Saint Ephraim the Syrian Eschatological Hymns and Homilies, translated by M.F. Toal and Henry Burgess, amended. (Florence, AZ: SAGOM Press, 2019). ISBN 978-1-9456-9907-8

d) Tafsiri ya Kihispania

  • San Efrén de Nísibis Himnos de Navidad y Epifanía, by Efrem Yildiz Sadak Madrid, 2016 ISBN 978-84-285-5235-6

Tanbihi

Vyanzo

  • Bou Mansour, Tanios (1988). La pensée symbolique de saint Ephrem le Syrien. Bibliothèque de l'Université Saint Esprit XVI. Kaslik, Lebanon.
  • Brock, Sebastian P (1985). The luminous eye: the spiritual world vision of Saint Ephrem. Cistercian Publications. ISBN 0-87907-624-0.
  • Brock, Sebastian (trans) (1990). Hymns on paradise: St. Ephrem the Syrian. St Vladimir's Seminary Press, Crestwood, New York. ISBN 0-88141-076-4.
  • den Biesen, Kees (2002). Bibliography of Ephrem the Syrian. Self-published, Giove in Umbria. (ephrem_bibliography@hotmail.com)
  • den Biesen, Kees (2006). Simple and Bold: Ephrem's Art of Symbolic Thought. Gorgias Press, Piscataway, New Jersey. ISBN 1-59333-397-8.
  • Griffith, Sidney H (1997). Faith adoring the mystery: reading the Bible with St. Ephraem the Syrian. Marquette University Press, Milwaukee, Wisconsin. ISBN 0-87462-577-7.
  • Matthews, Jr., Edward G. and Joseph P. Amar (trans), Kathleen McVey (ed) (1994). Saint Ephrem the Syrian: selected prose works. Catholic University of America Press. ISBN 0-8132-0091-1.
  • McVey, Kathleen E (trans) (1989). Ephrem the Syrian: hymns. Paulist Press. ISBN 0-8091-3093-9.
  • Mourachian, Mark. "Hymns Against Heresies: Comments on St. Ephrem the Syrian". Sophia, 17, No. 2, Winter 2007. ISSN 0194-7958.
  • Parry, Ken (1999). The Blackwell Dictionary of Eastern Christianity. Malden, MA.: Blackwell Publishing. ISBN 0-631-23203-6. {cite book}: Unknown parameter |coauthors= ignored (|author= suggested) (help)

Viungo vya nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu: