Flavia Domitila

Mchoro wa Andrea di Bonaiuto, "Mt. Agnes na Mt. Domitila", 1365. Galleria dell'Accademia, Florence.

Flavia Domitila alikuwa mwanamke wa ukoo wa kifalme huko Roma katika karne ya 1, binti wa Domitila Mdogo, akaolewa na binamu yake konsuli Titus Flavius Clemens[1].

Kwa kuwa alijiunga na Ukristo, alidhulumiwa kama mkanamungu na serikali ya Dola la Roma chini ya mjomba wake kaisari Domitian. Alipelekwa pamoja na wengine kwenye kisiwa cha Ponza alipoteseka hadi kufa.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 7 Mei (Ukristo wa magharibi)[2] au 12 Mei (Ukristo wa mashariki)[3].

Tazama pia

Tanbihi

  1. http://www.santiebeati.it/dettaglio/52100
  2. Martyrologium Romanum (Typis Vaticanis, 2nd edition, 2004), p. 274.
  3. Ἡ Ἁγία Δομιτίλλα ἡ Μάρτυς . 12 Μαΐου. ΜΕΓΑΣ ΣΥΝΑΞΑΡΙΣΤΗΣ.

Marejeo

  • Heinrich Grätz, Die Jüdischen Proselyten im Römerreiche, pp. 28 et seq.
  • idem, Gesch. 3d ed., iv. 403
  • Lebrecht, in Geiger's Jüd. Zeit. xi. 273
  • Berliner, Gesch. der Juden in Rom, p. 39
  • Kraus, Roma Sotterranea, p. 41, Freiburg-in-Breisgau, 1873
  • Reinach, Fontes Rerum, Judaicaram, i. 195
  • Prosopographia Imperii Romani, ii. 81.

Viungo vya nje

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.