Francesco Alciati

Francesco Alciati (2 Februari 152220 Aprili 1580) alikuwa askofu, kardinali na mtaalamu wa sheria kutoka Italia.

Wasifu

Francesco Alciati alizaliwa Milano tarehe 2 Februari 1522. Alikuwa jamaa wa mwanasheria mashuhuri Andrea Alciato na alisomea sheria chini ya mwongozo wake. Alciati alijipatia umaarufu haraka kama mmoja wa wasomi mashuhuri wa sheria huko Milano akapewa jina la utani l'Alciatino ili kumtofautisha na Andrea.

Katika wosia wake, Andrea Alciato alimteua Francesco kuwa mrithi wake akamkabidhi jukumu la kuhariri maandiko yake ambayo bado hayajachapishwa. Baada ya kifo cha Andrea, Francesco Alciati aliteuliwa kuwa profesa wa sheria za kiraia katika Chuo Kikuu cha Pavia. Mwanafunzi wake mashuhuri zaidi alikuwa Karoli Borromeo.[1]

Marejeo

  1. Sommar, Mary E. (2009). The Correctores Romani: Gratian's Decretum and the Counter-Reformation Humanists. Vienna: LIT Verlag. uk. 16. ISBN 978-3-643-90019-7.
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.