Fukusi

Fukusi
Kidungadunga wa mchele (Sitophilus oryzae)
Kidungadunga wa mchele (Sitophilus oryzae)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye miguu yenye viungo)
Nusufaila: Hexapoda (Wanyama wenye miguu sita)
Ngeli: Insecta (Wadudu)
Ngeli ya chini: Pterygota (Wadudu wenye mabawa)
Oda: Coleoptera (Wadudu wenye mabawa magumu)
Nusuoda: Polyphaga
Familia ya juu: Curculionoidea
Latreille, 1802
Ngazi za chini

Familia 7:

  • Anthribidae (Fukusi-viyoga) Billberg, 1820
  • Attelabidae (Fukusi wasokota majani) Billberg, 1820
  • Belidae (Fukusi wa kimsingi) Schönherr, 1826
  • Brentidae (Fukusi wenye domo-nyofu) Billberg, 1820
  • Caridae (Fukusi-misanduku) Thompson, 1992
  • Curculionidae (Fukusi wa kweli) Latreille, 1802
  • Nemonychidae (Fukusi wa maua ya misonobari) Bedel, 1882

Fukusi, vidungadunga au vipukusa ni wadudu wa familia ya juu Curculionoidea katika oda Coleoptera. Kuna familia 7 na moja, Curculionidae, ni baina ya familia kubwa kabisa yenye jenasi 6800 na spishi 83,000. Familia ya juu ina spishi 97,000. Pengine familia mbili nyingine zinatambuliwa, Platypodidae na Scolytidae, lakini siku hizi hupatiwa cheo cha nusufamilia, ijapokuwa njia ya maisha yao ya kupukusa katika ubao imegeuza umbo lao sana.

Maelezo

Sifa bainifu ya fukusi ni domo refu lenye sehemu za kinywa kwenye ncha yake. Ukubwa wao unatofautiana kutoka mm 1 hadi 40. Vipapasio vya spishi nyingi sana vimepindika kama kisugudi, lakini fukusi wa kimsingi wana vipapasio nyofu.

Lava za fukusi hula tishu za mimea, miti au viyoga au mbegu zao. Wapevu hula maua, matunda, mbelewele, viyoga na kwa nadra wadudu, kama vile wadudu-gamba.

Kama chakula

Lava za fukusi, zile kubwa hasa, huliwa mahali pengi pa dunia. Zinaweza kuliwa mbichi, zilizopikwa, zilizokaangwa au zilizobanikwa.

Spishi zilizochaguliwa za Afrika ya Mashariki

  • Alcidodes leucogrammus, Fukusi Milia wa Mkunde
  • Aperitmetus brunneus, Fukusi wa Mizizi ya Mchai
  • Araecerus fasciculatus, Kidungadunga wa Buni
  • Cosmopolites sordidus, Fukusi wa Mgomba
  • Cylas formicarius, Fukusi wa Kiazi Kitamu
  • Euwallacea xanthopus, Kipukusa wa Msandarusi
  • Hypolixus haerens, Fukusi wa Mchicha
  • Neochetina bruchi, Fukusi wa Yasinthi-maji
  • Rhynchophorus phoenicis, Sururu
  • Sitophilus oryzae, Kidungadunga wa Mchele
  • Sitophilus zeamais, Kidungadunga wa Mahindi
  • Sphrigodes mixtus, Fukusi wa Nyambene
  • Sternochetus mangiferae, Fukusi wa Maembe
  • Xylosandrus crassiusculus, Kipukusa Ambrozia wa Asia

Picha