Guru

Kwa mwimbaji anayetumia jina hili tazama Guru (rapa)

Guru (Kisanskrit गुरु guru - mzito, mkubwa) ni neno la lugha ya Kisanskrit amabalo katika dini zenye asili ya Uhindi kama Ubuddha na Uhindu lamaanisha mwalimu wa kiroho.

Katika utamaduni wa Kihindi mwenye kutafuta ukweli au mwangaza wa kiroho anamtegemea kiongozi au mwalimu atakayemwongoza kwenye njia ya kiroho. Huyu anajulikana kwa cheo cha "guru".

Katika dini ya Kalasinga "Guru" ni cheo cha viongozi 10 wa kwanza walioanzisha na kuongoza imani hii. Tangu mwaka 1708 hakuna guru wa kibinadamu tena kati ya Kalasinga na kitabu kitakatifu chao kinaheshimiwa kama guru kwa jina la Guru Granth Sahib.

Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.