Hafiz
Hafiz (kutoka Kiarabu حافظ ḥāfiẓ -kitenzi حفظ ḥāfaẓa = "kuhifadhi, kutunza") ni cheo cha heshima katika Uislamu kwa kumtaja mtu aliyeishika Kurani yote moyoni. Mwanamke au binti aliyeishika msahafu huitwa "hafiza".
Hafiz anajua kusema maneno yote ya Kurani. Mtu wa aina hii huheshimiwa sana kati ya Waislamu. Mara nyingi ni watu vipofu au walemavu wanaoanza kushika maneno ya Kurani tangu utoto maana kwao ni njia mmoja ya kuheshimiwa pia kuwa na mapato kwa sananu mahafiz hualikwa mara nyingi kuimba surat za Kurani wakati wa sherehe na siku maalumu.
Mahafiz wa kwanza wanasemekena walitokea katika siku za kwanza za Uislamu kwa sababu mwanzoni Kurani ilitangazwa na mume Muhammad kama hotuba tu hapakuwa na utaratibu wa kuiandika. Lakini watu wengi walishika maneno haya. Baadaye Khalifa Umar aliagiza Kurani yote kuandikwa na katika kazi hii mahafiz walikuwa muhimu walioweza kurudia surat kwa waandishi.
Hata baada ya Kurani iliandikwa bado mahafiz walitafutwa kwa sababu Waislamu wengi hawakujua kusoma tena kwa sababu namna yao ya kuimba maneno ya surat uliwavuta watu. Kati ya watoto wanaoanza kujifunza Kurani katika madrasa wanjitokeza mara kwa mara kadhaa wanaoelekea kuwa hafiz.
Kutokana na heshima ya cheo hiki kimetumiwa mara nyingi kama jina kati ya Waislamu ikiandikwa pia Hafez, Hafes, au Hafis kutegemeana na lugha ya mazingira.