Historia Kuu ya Afrika

Kikao cha kamati ya Kisayansi ya UNESCO kwa Historia Kuu ya Afrika, Juni 2010

Historia Kuu ya Afrika (kwa Kiingereza w: General History of Africa (GHA)) ni mradi wa UNESCO ulioanzishwa tangu mwaka 1964.

Shabaha ya mradi ni kusahihisha “maelezo mapotovu yaliyokuwa yakieleza umaskini na ushenzi katika bara hili” kwa “kufanya uchunguzi mwafaka wa habari usiokuwa na upendeleo” . Uliona Historia ya Afrika “imeharibiwa mno kutokana na kutokujua na ubinafsi wa watu walioiandika” [1] .

Awamu ya kwanza hadi mwaka 1999 ilikuwa kuandika na kutoa vitabu 8 kuhusu Historia Kuu ya Afrika.

Awamu ya pili tangu mwaka 2009 inalenga kuandaa muhtasari wa historia na vitabu pamoja na misaada kwa walimu wa shule.

Vitabu vya Historia Kuu ya Afrika

Toleo la Kiingereza la Historia Kuu ya Afrika
Profesa Joseph Ki-Zerbo, mhariri mkuu wa kitabu I cha Historia Kuu ya Afrika

Vitabu vinane vilivyotolewa vimeandikwa na wataalamu mbalimbali kutoka Afrika na nje yake na kutolewa kwa lugha mbalimbali, zikiwa pamoja na Kiswahili[2]. Vimetolewa mara mbili kama juzuu kamili na juzuu lililofupishwa.

Vyote vinane vya juzuu lililofupishwa vinapatikana kwa njia ya intaneti kwenye tovuti ya UNESCO. Hapa tunonyesha nakala za Kiswahili; viungo kwa nakala za Kiingereza zinapatikana kwenye makala pacha ya Kiingereza.

  • Kitabu cha Pili: Staarabu za Kale za Afrika
    Mhariri mkuu G. Mokhtar, online kwa Kiingereza, Kiarabu, Kireno, Kihausa, Kiswahili na Kifulfulde
  • Kitabu cha Nane: Afrika tangu 1935
    Wahariri wakuu A.A. Mazrui and C. Wondji, online kwa Kiingereza, Kiarabu, Kireno, na Kiswahili

Tanbihi

  1. Utangulizi wa jumla, uk 1 HKA Kitabu cha Kwanza
  2. TUKI-UNESCO, Historia Kuu ya Afrika, I-VIII, Dar es Salaam, 1999, ISBN 9976 911 40 8
Makala hii kuhusu kitabu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Historia Kuu ya Afrika kama Mwandishi wake, hadithi au matoleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.