Jiji la Zanzibar
Jiji la Zanzibar | |
Mahali pa mji wa Zanzibar katika Tanzania |
|
Majiranukta: 6°9′36″S 39°12′0″E / 6.16000°S 39.20000°E | |
Nchi | Tanzania |
---|---|
Mkoa | Unguja Mjini Magharibi |
Wilaya | Unguja Mjini |
Jiji la Zanzibar ni mji mkubwa wa kisiwa cha Unguja na mji mkuu wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.
Pia ni wilaya katika Mkoa wa Unguja Mjini Magharibi wa Tanzania.
Jiji lina wakazi 206,292 (sensa ya mwaka 2002).[1]
Jina
- Makala kuu: Etimolojia ya Neno Zanzibar
Mji Mkongwe
Kitovu cha historia yake ni Mji Mkongwe (Stone Town) ulioandikishwa katika orodha ya UNESCO ya "Urithi wa Dunia" (World Heritage).
Nyumba za Mji Mkongwe zilijengwa tangu mwaka 1830 wakati Sultani Sayyid Said alipohamisha mji mkuu wake kutoka Omani kuja Unguja.
Kati ya majengo maarufu ni Beit al Ajaib (yaani Jumba la Maajabu lililobomoka tarehe 24 Desemba 2020[2]), boma la kale, Kanisa Kuu la Kianglikana lililojengwa mahali pa soko la watumwa na hasa nyumba nyingi za kihistoria za ghorofa zilizojengwa na famila za tabaka la matajiri Waarabu zenye milango yenye mapambo mazuri.
Mji Mkongwe unapokea watalii wengi kila mwaka.
Mji wa kisasa umekua sana ng'ambo ya Mji Mkongwe.
Tazama Pia
Picha
-
Nyumba ya Maajabu (Beit-al-Ajaib
-
Boma la Kale katika Mji Mkongwe
-
Mahalipa kuogelea ufukoni karibu na Mji Mkongwe
Marejeo
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2004-03-18. Iliwekwa mnamo 2004-03-18.
- ↑ https://www.mwananchi.co.tz/mw/habari/kitaifa/jengo-la-kihistoria-beit-al-ajaib-laanguka-zanzibar-3239382
Viungo vya nje
Stone Town travel guide kutoka Wikisafiri
- Historia na utamaduni wa Zanzibar Ilihifadhiwa 7 Februari 2006 kwenye Wayback Machine.
- UNESCO Stone Town Site
- Stone Town Conservation and Development Authority Ilihifadhiwa 22 Oktoba 2016 kwenye Wayback Machine.
- Zanzibar Urban District Homepage for the 2002 Tanzania National Census Ilihifadhiwa 18 Machi 2004 kwenye Wayback Machine.
- Stranger in Paradise: Searching for a Place to Call Home in Stone Town Ilihifadhiwa 18 Julai 2011 kwenye Wayback Machine. by Christopher Vourlias, World Hum, June 15, 2009
- Zanzibar Stone Town & Hotels Ilihifadhiwa 11 Juni 2011 kwenye Wayback Machine. A travel guide website containing pictures and information about Stone Town as well as a selection of Stone Town Hotels.
- Stone Town sites and attractions Ilihifadhiwa 16 Machi 2012 kwenye Wayback Machine.
Kata za Wilaya ya Mjini Unguja - Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja - Tanzania | ||
---|---|---|
Amani | Banko | Chumbuni | Gulioni | Jang'ombe | Karakana | Kidongo Chekundu | Kikwajuni Bondeni | Kikwajuni Juu | Kilimahewa Bondeni | Kilimahewa Juu | Kilimani | Kiponda | Kisimamajongoo | Kisiwandui | Kwaalimsha | Kwaalinatu | Kwabintiamrani | Kwahani | Kwamtipura | Kwamtumwajeni | Kwa Wazee | Magomeni | Makadara | Malindi | Mapinduzi | Maruhubi | Masumbani | Matarumbeta | Mboriborini | Mchangani | Meya | Miembeni | Migombani | Mikunguni | Mitiulaya | Mkele | Mkunazini | Mlandege | Mnazimmoja | Mpendae | Muembeshauri | Muembetanga | Muungano | Mwembeladu | MwembeMadema | Mwembemakumbi | Nyerere | Rahaleo | Saateni | Sebleni | Shangani | Shaurimoyo | Sogea | Urusi | Vikokotoni |
Makala hii kuhusu maeneo ya Unguja bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Zanzibar (Jiji) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno. |