Karne XIII
Lango la Historia | Lango la Biografia | Karibuni | Orodha ya Miaka
◄ |
Karne ya 11 |
Karne ya 12 |
Karne ya 13
| Karne ya 14
| Karne ya 15
| ►
Miaka ya 1200 |
Miaka ya 1210 |
Miaka ya 1220 |
Miaka ya 1230 |
Miaka ya 1240 |
Miaka ya 1250 |
Miaka ya 1260 |
Miaka ya 1270 |
Miaka ya 1280 |
Miaka ya 1290
Karne ya 13 ilikuwa kipindi cha miaka mia moja kati ya 1201 na 1300. Kikamilifu kilianza tarehe 1 Januari 1201 na kuishia 31 Desemba 1300. Namba zake zinafuata hesabu ya miaka "baada ya Kristo".
Kama kila "karne" ni kipindi kinachohesabiwa kwa hiari ya kibinadamu kwa sababu ni mgawanyo wa kalenda tu: katika hali halisi maendeleo na mabadiliko makubwa hayafuati migawanyo ya kalenda ya kibinadamu.
Kuna mambo mengi yaliyotokea wakati wa karne hii, kama haya yafuatayo.
Watu na matukio
- Gengis Khan (1162 - 1227), anaanzisha kipindi cha pax mongolica, Ulaya inafanya biashara na China
- Konstantinopoli unatekwa na watu wa Ulaya magharibi: mwanzo wa Ufalme wa Kilatini wa mashariki
- Miji yenye bahari ya Italia inatawala Bahari ya Mediteranea, hasa Venezia
- Zinaanza benki
- Falme za kitaifa zinajitokeza Ulaya
- Kaisari Federiko II anastawisha sanaa akitawala huko Palermo (Sisilia)
- Papa Inosenti III anafikisha mamlaka ya Papa upande wa siasa kwenye kilele chake
- Inastawi sanaa ya Kigoti
- Ukoo wa Wapaleologi unakomboa Konstantinopoli na kuleta hali mpya ya ustawi
- Marko Polo (Venezia, 1254 - 1324), mfanyabiashara na mvumbuzi huko China
- Fransisko wa Asizi (Asizi, 1182 hivi - 1226), mwanzilishi wa Wafransisko
- Dominiko wa Guzman kuanzisha shirika la Wahubiri
- Toma wa Akwino (1225 hivi - 1274), anafikisha elimu ya Skolastika kwenye kilele chake
- Huko China wanabuni dira