Kifrisia

Kifrisia ni lugha ya kundi la watu wanaoishi katika Uholanzi ya mashariki na Ujerumani ya Kaskazini karibu na pwani ya Bahari ya Kaskazini katika maeneo ya Frisia ya kihistoria, yakiwa pamoja na mkoa wa Friesland wa Uholanzi, wilaya ya Friesland katika Saksonia Chini, Ujerumani na wilaya ya Nordfriesland (Frisia Kaskazini) katika Schleswig-Holstein, Ujerumani.

Lugha hiyo ni lugha ya Kigermanik iliyo karibu na Kiingereza katika lugha za Kihindi-Kiulaya.

Idadi ya wasemaji imepungua, na leo hii wakazi wengi wa maeneo ya Frisia wanatumia ama Kiholanzi na Kijerumani au lahaja mojawapo ya Kijerumani cha Kaskazini.

Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kifrisia kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.