Kilovolti

Kilovolti ni kizio cha SI kwa volteji ya umeme. Alama yake ni kV. Kilovolti moja ni sawa na 103 V, au volti 1000.

Kilovolti moja ni takriban mara 4 ya volteji inayotumiwa katika nyumba za nchi nyingi. Katika Afrika ya Mashariki (sawa na Ulaya na nchi nyingi za Asia) gridi ya taifa ya umeme inatumia volteji za kV 66 hadi kV 400 kwenye njia za ugawaji wa umeme nchini[1].

Marejeo

  1. Transmission Ilihifadhiwa 16 Februari 2022 kwenye Wayback Machine., Tovuti ya Tanesco, iliangaliwa Februari 2022