Golikipa

Michael Rensing, golikipa wa FC Bayern Munich.
Alison Becker, mlinda lango wa timu ya Liverpool FC na timu ya taifa ya Brazili

Golikipa (kutoka Kiingereza "goalkeeper"; pia kipa tu; kwa jina lingine mlinda lango) ni mchezaji maalumu ambaye hulinda lango la timu katika michezo mingi kama soka na hockey inayohusisha kufunga katika lango.

Kazi ya kipa ni kuzuia timu pinzani kufunga bao kwa kuingiza mpira golini. Yaani yeye anayepewa jukumu la kuzuia timu pinzani kufunga goli katika lango lake.

Nafasi hii ni mahususi katika michezo ya Soka, bandy, rink bandy, camogie, Gaelic football, Mpira wa sakafu, mpira wa mikono, hockey, polo na michezo mingine mingi.

Katika michezo mingi inayohusisha kufanga katika wavu, sheria maalumu huwekwa kwa mlinda lango tofauti na wachezaji wengine. Sheria hizo hulenga kunlinda golikipa dhidi ya hatari na vitendo vyenye athari kwake.

Hii inaweza kuonekana sanasana katika mchezo wa hokey ambapo golikipa huvaa mavazi maalumu kama kofia ngumu ili kumlinda na vishindo kutokana na kugongwana vitu vigumu kama fimbo ya kuchezea na mpira.

Baadhi ya michezo, golikipa hufuata sharia kama wachezaji wengine, mfanoi, katika mchezo wa soka, anaweza kupiga mpira kwa miguu kama wachezaji wengine, lakini pia anaweza kutumia mikono yake ila kwenye eneo maalumu tu. Baadhi ya michezo golikipa hana uhuru wa kucheza uwanja mzima, na baadhi ya matendo hawezi kufanya akiwa nje ya eneo linaloruhusiwa.

Mifano

Mpira wa mikono

Katika mpira wa mikono, golikipa pekee ndie anayeruhusiwa kukaa eneo la mita 6 kuzunguka lango lake kwa kipindi chote cha mchezo. Golikipa anaruhusiwa kuzuia mpira kutumia sehemu yoyote ya mwili iwe miguu, mikono hata kichwa ila tu akiwa eneo la mita sita kutoka langoni kwake.

Mpira ukigusa chini eneo la mita sita wakati wa mchezo, golikipa tu ndie anayeruhusiwa kuucheza aidha kwa kuupiga au kuushika, mpira ukiwa eneo la mita sita lakini haujagusa chini, mchezaji yeyote anaruhusiwa kuucheza ila tu asiwe amegusa chini, anaweza fanya hivyo kwa kuruka na kupiga mpira akiwa hewani.

Golikipa anaweza kuhusika kwenye ushambuliaji kwa kurusha pasi ndefu upande wa nusu ya pili ya uwanja kwa kutoa psi kwa mchezaji mwenza.

Mavazi ya kawaida ya golikipa wa mpira wa mikono:

  • Jezi ya mikono mirefu
  • Suruali ndefu
  • Mavazi mengineyo ya kumkinga

Soka

golikipa kijana wa umri mdogo

Katika Soka, golikipa wa kiula timu ana jukumu la kulinda langop la timu yake wakati wa mchezo na hua na upendeleo wa kipekee tofauti na wachezaji wengine. Kazi kuu ya golikipa ni kuzuia mpira usiingie katika lango lake na ndiye mchezaji pekee anayeruhusiwa kutumia mikono yake kushika, kurusha au kuzuia mipira ila tu akiwa katika eneo la penati. Kisheria anatakiwa kuvaa jezi ya rangi tofauti na wachezaji wenzake na refa, hii ni ili kumsaidia refa kumtambua kwa urahisi. Hakuna mahitaji mengine maalumu japo wanaruhusiwa pia kuvaa vifaa vya ziada vya kuwakinga. Magolikipa wengi huvaa glovu pia, glovu hulinda mikono yao na pia kuongeza uwezo wa kushika mpira.

Golikipa anaruhusiwa kushika mpira na pia kuupangua mpira uliolenga lango. Mara kadha, golikipa huwa na faida zaidi katika mipira iliyopo hewani kwani anaweza kuruka na kunyoosha mikono yake kabla mshambuliaji hajaucheza kwa kichwa. Golikipa akiushika mpira, anaruhusiwa kuupiga kwa mguu, kuurusha au kuuweka chini na kuucheza kwa mguu. Katika sharia za soka, golikipa anaposhika mpira, ni lazima autoe katika himaya yake ndani ya sekunde sita, lakini refa anaweza kuamua muda wa kuruhusu golikipa kuushoika mpira iwapo tu hatakua na nia ya kupoteza muda. Golikipa akishika mpira, wachezaji wa timu pinzani hawaruhusiwa kugusa mpira huo na ni lazima kutoa nafasi kwa golikipa kuucheza mpira huo. Mpira ukiwa hewani na mchezaji wa timu pinzani akawa anaugombea na golikipa, golikipa hupata upendeleo kwani hana nafasi ya kujikinga.

Japokua golikipa anaruhusiwa kushika mpira kwa mikono akiwa katika eneo linaloruhusiwa, hii inakua tofauti akipewa pasi na mchezaji mwenzake, Ktika hali ya namna hiyo, itamlazimu golikipa kucheza mpira kwa miguu ila hawezi kunyanyua mpira. Sheria hii ni kwa pasi iliyotolewa kwa mguu tu, pasi za vichwa au kwa namna yoyote isiyohusisha mguu anaweza kunyanyua kwa mikono. Akivunja sharia hiyo timu inapata adhabu ya pigo lisilo la moja kwa moja

Kwa kuwa golikipa ndiye mchezaji pekee kwenye timu mwenye uwezo wa kuona uwanja mzima, mara kadhaa ndiye anayeelekeza wachezaji wakati wa kukaba hasa mapigo ya mipira iliyokufa kuelekea langoni kwake. Hii inamaanisha golikipa lazima awe na sauti ya kutosha kuwaelekeza walinzi wake na walinzi wake inawapasa kusikilia na kufuata anachowaelekeza golikipa.

Netiboli

Katika netiboli, golikipa huvaa jezi yenye herufi GK, kisheria, lazima abaki katika robo tatu ya kiwanja kwa upande wa goli lao lilipo. Golikipa ni miongoni mwa wachezaji wane wanaopruhusiwa kuingia katika duara la kufunga, pamoja nae GD, GS na GA wanaweza kuingia. Mara kadha, goliki[pa humkaba GS wa timu pinzani.

Kipa kwenye sarafu na stampu

Magolikipa wamekua wakitumika na baadhi ya wakusanyaji wa sarafu na medali, mfano sarafu ya euro 5 ya Austria ambayo ilichongwa 12 Mei 2004. Sarafu hiyo inaonesha shuti lililopigwa na mchezaji anayeonekana kwa mbali ambalo linampita golikipa (likiwa bado lipo hewani) kuelekea golini.

Viungo vya nje

Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu Golikipa kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.