Kivuli

Wakati wa jioni kivuli huwa ndefu

Kivuli ni eneo lenye nuru kidogo katika mazingira yenye nuru zaidi. Kinapatikana nyuma ya gimba kinachoangazwa upande moja lakini kinazuia nuru kuendelea na hivyo kuunda eneo lenye giza au nuru kidogo nyuma yake.

Kila kitu kisichopitisha nuru ndani chake kinaweza kuwa na kivuli kikianganzwa upande mmoja. Mfano wa gimba ambalo halina kivuli ni hewa au pia kioo safi dirishani.

Kwa maana pana zaidi kuna pia kivuli cha mnururisho usio nuru ya kuona kwa macho; mata ogania ndani ya mwili unapitisha au kuzuia mnururisho wa eksirei kwa viwango tofauti na kuonekana baadaye kwenye picha kwa rangi tofauti kutokana na "kivuli" dhidi ya mionzi hii.

Ukubwa na umbo la kivuli

Ukubwa wa kivuli unategemea umbali wa gimba lenye kivuli na chanzo cha nuru. Kama gimba liko karibu na chanzo cha nuru kivuli huwa kubwa zaidi, kama liko mbali kivuli huwa kidogo. Ukiweka mkono karibu na tochi kivuli chale huwa ni kikiubwa, kadri unavyopeleka mkono mbali na tochi kivuli chake kinapungua.

Kivuli kamili (A) na nusu kivuli (B) kutokana na vyanzo viwili vya nuru (N1 + N2)

Vilevile umbo la kivuli unategemea pembe ya kijiometria kati ya chanzo cha nuru na gimba. Hii inaonekana kwa kuzatama kivuli cha mtu au nyumba wakati wa mchana na wakati wa jioni. Jioni jua linaonekana chini zaidi angani hivyo pembe la nuru yake ni dogo na kivuli kirefu. Kama jua liko juu kabisa angani kivuli huwa ndogo maana nuru inafika kutoka pande nyingi, hivyo kivuli ina nafasi ndogo tu, ni "fupi". Kama jua liko "chini" wakati wa asubuhi au jioni linaangaza upande moja tu hivyo nafasi ya kivuli inakua.


Aina za vivuli

Kama chanzo cha nuru kinafanana na nukta kivuli ni kali yaani kuna kivuli kamili tu kinachokaribia rangi nyeusi. Tofauti kati ya kivuli na eneo lenye nuru ni kali kama mstari uliochorwa. Lakini kama chanzo cha nuru ni pana zaidi kuna ngazi mbili za kivuli yaani kivuli kamili (en:umbra) na nusu kivuli (penumbra). Kati ya nusu kivuli na maeneo yenye nuru mpaka si kali tena.

Mchezo wa Kivuli huko Bali, Indonesia

Hali ya nusu kivuli inatokea pia kama gimbe lilelile linaangazwa na vyanzo viwili vya nuru.

Kama chanzo cha nuru ni pana sana kama anga iliyofunikwa na mawingu kivuli kinaweza kupotea kabisa. Maana kiasi cha nuru inatokea kote angani.

Kivuli na sanaa

Tangu kale watu walitumia kivuli kwa mchezo na kutumia matokeo yake katka uchoraji. Mchezo unaopendwa ni kupeleka mkono mbele ya chanzo cha nuru kama mshumaa au taa na kuunda kivuli kinachofanana na uso au mnyama fulani. Katika nchi nyingi wasanii waliendelea kutumia maumbo ya watu, wanyama na vitu vingine vilivyokatwa katika karatasi na kuleta sura ya umbo kwenye kitambaa cheupe yakiangaziwa na nuru kwa nyuma.



Picha za viwuli

Viungo vya Nje

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons