Krisanto na Daria
Krisanto na Daria (walifariki 283 hivi) ni mume na mke Wakristo waliopata umaarufu tokea zamani kama wafiadini[1], ambao juu ya makaburi yao mjini Roma limejengwa kanisa.[2]
Krisanto alitokea Aleksandria (Misri) na kuhamia Roma kwa ajili ya masomo. Baada ya kufahamiana na padri Karpoforo, alibatizwa akaleta wengi kwa Yesu Kristo[3], mmojawao Daria[4].
Hatimaye walizikwa hai katika dhuluma ya kaisari Numeriani wakiwa bado vijana[5].
Papa Damaso I aliwasifu kwa shairi na Gregori wa Tours vilevile katika kitabu "De Gloria Martyrum" [6]
Wanaheshimiwa na Wakatoliki, Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki kama watakatifu.
Sikukuu yao inaadhimishwa tarehe 25 Oktoba[7] au 19 Machi.
Tazama pia
- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
- ↑ Martyrologium Hieronymianum
- ↑ "Sts. Chrysanthus and Daria". Catholic Encyclopedia, 1908. new advent.org. Iliwekwa mnamo 10 Mei 2013.
{cite web}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ https://www.santiebeati.it/dettaglio/92161
- ↑ https://www.santiebeati.it/dettaglio/92162
- ↑ https://web.archive.org/web/20130210082116/http://www.nationalgeographic.it/popoli-culture/2011/04/14/foto/csi_reliquie_il_mistero_dei_martiri-288829/1/#media
- ↑ P. Migne, in Patrologia Latina, vol. LXXI, col. 739.
- ↑ Martyrologium Romanum
Viungo vya nje
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
- Catholic Encyclopedia: Sts. Chrysanthus and Daria
- Patron Saints Index: Sts. Chrysanthus and Daria Ilihifadhiwa 29 Novemba 2005 kwenye Wayback Machine.
- Holy Protection Russian Orthodox Church
- Holy Martyrs Chrysanthus and Daria in Orthodoxy Ilihifadhiwa 4 Februari 2012 kwenye Wayback Machine.
- Selected Lives of Saints
- The Two Lovers of Heaven: Chrysanthus and Daria at Project Gutenberg. A drama of early Christian Rome by Pedro Calderón de la Barca, translated by Denis Florence MacCarthy.
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |