Kura

Huko Uswisi, kura zinapigwa mara nne kwa mwaka: kila raia analetewa nyumbani maelezo na vifaa vya kupigia kura.

Kura ni tendo au njia ya kawaida kwa kundi la watu ama kuchagua kiongozi wanayemtaka ama kuchukua maamuzi wanayoona yanafaa.

Taratibu za kupiga kura zinaweza kuwa mbalimbali, kwa mfano kuhusu nani apige, nani apigwe kura, kwa namna gani n.k.: mara nyingi ni muhimu itunzwe siri kuhusu kura iliyotolewa na kila mtu, aweze kuitoa bila hofu au shuruti kutoka nje.

Demokrasia inapenda chaguzi zifanyike na maamuzi mengi yachukuliwe baada ya mjadala mpana na kura za wengi.

Pengine kupiga kura ni wajibu unaosisitizwa na sheria, lakini mara nyingi zaidi mwenye haki ya kupiga kura anaweza kuachiwa hiari asiitumie, tena dini ndogo chache zinakataza waumini wasipige kura kamwe.

Viungo vya nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mambo ya sheria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kura kama historia yake au uhusiano wake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.