Kwarara

Kwarara
Kwarara shingo-nyeusi
Kwarara shingo-nyeusi
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Pelecaniformes (Ndege kama wari)
Familia: Threskiornithidae (Ndege walio na mnasaba na kwarara)
Nusufamilia: Threskiornithinae (Ndege wanaofanana na kwarara)
Poche, 1904
Ngazi za chini

Jenasi 13:

  • Bostrychia G.R. Gray, 1847
  • Cercibis Wagler, 1832
  • Eudocimus Wagler, 1832
  • Geronticus Wagler, 1832
  • Lophotibis Reichenbach, 1853
  • Mesembrinibis J.L. Peters, 1930
  • Nipponia Reichenbach, 1853
  • Phimosus Wagler, 1832
  • Plegadis Kaup, 1829
  • Pseudibis Hodgson, 1844
  • Thaumatibis Elliot, 1877
  • Theristicus Wagler, 1832
  • Threskiornis G.R. Gray, 1842

Kwarara ni ndege wa nusufamilia Threskiornithinae katika familia Threskiornithidae ambao wana miguu mirefu. Domo refu lao limepindika na hutumika kwa kutafuta chakula ndani ya matope. Spishi nyingi za kwarara huweka matago yao juu ya miti, kwa kawaida pamoja na yange, koikoi au domomwiko. Jike huyataga mayai 2-4.

Spishi za Afrika

Spishi za mabara mengine

Picha