Lalibela, Ethiopia
Lalibela ni mji unaopatikana kaskazini mwa Ethiopia. Ni mmoja kati ya miji mitakatifu nchini humo.
Mji huu ni wa pili kwa utakatifu ukifuatia ule wa Aksum, na pia ni patakatifu kwa ajili ya kufanyia hija kwa wakazi wengi wa nchini Ethiopia.
Tofauti na mji wa Aksum, watu wengi katika mji wa Lalibela kwa ujumla ni Wakristo Waorthodoksi wa Mashariki. Lalibela ilikusudiwa kuwa Yerusalemu mpya kama matokeo ya mji wa Yerusalemu kuchukuliwa na Waislamu. Hata majina kadhaa katika kanisa la Lalibela yametokana na majengo mbalimbali katika mji wa Yerusalemu.
Likiwa linapatikana katika ukanda wa Semien Wollo (Semien Wollo Zone) wa kabila la Amhara au Kilil mita 2.500 juu ya usawa wa bahari.
Kutokana na takwimu za serikali, mwaka 2005, mji wa Lalibela ulikadiriwa kuwa na idadi ya watu wapatao 14,668 ambao kati yao, 7,049 ni wanaume na 7,619 ni wanawake. [1]. [2]
Katika Lalibela pia kunapatikana uwanja wa ndege wa Lalibela unaoitwa Lalibela Airport (Kodi ya ICAO HALL, IATA LLI), soko kubwa, shule na hospitali moja.
Historia
Katika kipindi cha uongozi cha Mtakatifu Gebre Mesqel Lalibela (aliyekuwa wa nasaba ya Zangwe, iliyoongoza kuanzia karne ya 12 hadi karne ya 13) mji wa sasa wa Lalibela ulikuwa ukijulikana kama Roha. Mfalme huyo mtakatifu aliupa mji huo jina hilo kutokana na mambo yaliyotokea wakati wa kuzaliwa kwake, ambayo ndiyo yaliyomfanya mama yake kujua mambo yatakayotokea katika maisha yake ya baadaye kama mfalme wa Ethiopia (Negus).
Majina ya sehemu mbalimbali katika mji wa Lalibela yanatokana na majina mbalimbali ambayo Mfalme huyo aliyapata alipokwenda katika mji wa Yerusalemu ambao ni mji mtakatifu (Holly Land) alipokuwa kijana. Lalibela anaonekana kuuona mji wa Yerusalame na kujaribu kujenga Yerusalemu Mpya kutokana na mji mkongwe wa Yerusalemu kuchukuliwa na Waislamu mwaka 1187.
Kutokana na hali hiyo, mambo mengi ya asili katika mji huo yanatokana na majina ya Biblia, hata jina la mji wenyewe unaojulikana kama Mto Yordani. Ulibaki kuwa mji mkuu wa Ethiopia tangu karne ya 12 na karne ya 13.
Mtu wa kwanza kutoka katika bara la Uropa kufika katika kanisa hili, alikuwa mpelelezi wa Ureno aliyeitwa Pêro da Covilhã (1460 – 1526). Padri wa Kireno aliyeitwa Francisco Álvares (1465 - 1540), alikuwa amesindikizwa na balozi wa Ureno wakati alipotembelea Lebna Dengel mwaka 1520. Katika maelezo yake kuhusiana na miundo aliatamka kwamba, “Nachoka kuandika zaidi juu ya haya majengo, kwa sababu inaonekana kwangu kuwa sitaaminika kama nitaongea zaidi… Naapa kwa Mungu, ambaye ni kwa nguvu zake kwamba mimi nipo, kuwa kila nilichokiandika ni ukweli”.[3]
Japokuwa Ramuso alijumuisha mipango ya makanisa mengine ya aina hii katika kitabu chake cha Alvares, haijajulikana bado, ni nani aliyempa hiyo michoro. Mtu mwingine aliyeripotiwa kutembelea Lalibela alikuwa Miguel de Castanhoso, aliyekuwa mwanajeshi chini ya Christovão da Gama na kuondoka katika nchi ya Ethiopia mwaka 1544. [4]. Baada ya Castanhoso, zaidi ya miaka 300 ilipita hadi Mzungu mwingine, Gerhard Rohlfs, alipotembelea tena Lalibela muda fulani kati ya miaka 1865 na 1870.
Kwa mujibu wa Futuh al-Habasa wa Sihab ad-Din Ahmad, Ahmad Gragn alichoma moja ya makanisa ya Lalibela katika uvamizi wake nchini Ethiopia.[5]. [6][7][8]
Makanisa
Eneo hili la kijiji linajulikana duniani kwa makanisa mbalimbali kama vile "kanisa la mwamba mmoja" ambalo linakuwa moja ya sehemu muhimu katika historia ya teknolojia ya ukataji miamba. Tarehe halisi ya kuanzishwa kwa makanisa hayo, haijarekodiwa vizuri, lakini wengi wanajua kuwa yamejengwa katika kipindi cha uongozi wa Lalibela, hasa karne ya 12 na karne ya 13. Makanisa hayo yameorodheshwa na UNESCO kama urithi wa dunia.
Kuna makanisa yapatayo 13, ambayo yapo pamoja katika makundi manne:
Kundi la Makanisa ya upande wa kaskazini: Bete Medhane Alem ambapo ni nyumbani kwa Msalaba wa Lalibela ambalo ndilo linaloaminika kuwa kubwa kuliko yote ya namna hiyo duniani, pengine nakili ya lile la Mtakatifu Maria wa Zion St. Mary of Zion la Aksum. Limeungana na kanisa la Bete Maryam (pengine kanisa kongwe kuliko yote). Bete Golgotha (linalojulikana kama lenye Kaburi la Mfalme wa Lalibela) kanisa dogo la Selassie na kaburi la Adam.
Kundi la Makanisa ya Magharibi: kanisa la Mtakatifu George, Bete Giyorgis, linasemekana kuwa ndilo kanisa linaloongoza kwa michoro mizuri na ndilo kanisa lilituzwa vizuri zaidi.
Kundi la Makanisa ya Mashariki: ni pamoja na kanisa la Bete amanuel (pengine ndilo kanisa la kwanza la kifalme) na (pia linawezekana kuwa gereza la kwanza) Bete Abba Libanos na Bete Gabriel-Rufael (pengine nyumba ya kwanza ya kifalme) linalohusishwa na utakatifu bakery.
Zaidi eneo lililopo katika monasteri ya Ashetan Maryan na kanisa la Yimrehane Kristos (pengine kanisa la kumi na moja, lilijengwa katika mtindo wa Aksum, lakini ndani ya pango.
Kumekuwa na mkanganyiko katika suala la lini hasa makanisa haya yalijengwa, David Buxton alianzisha uhesabuji wa pamoja na uliokubaliwa wa uhesabuji wa miaka kihistoria, na kueleza kuwa, “mawili kati yao yanafuata, katika hesabu za hakika, zilizowasilishwa na Debra Damo na kusahihishwa na Yemrahana Kristos."[9]
Muda uliotumika katika kutengeneza mapango haya kutoka katika miamba ya kawaida, hakuna shaka ni kiasi cha miongo kadhaa ya uongozi wa mfalme Lalibela. Boxtons anawaza kuwa kazi iliweza kufika hadi karne ya 14. [10]. Hata hivyo, David Phillipson, profesa wa sayansi ya miamba katika chuo kikuu cha Cambridge, anashauri kuwa, makanisa ya Merkoris, Gabriel-Rufael na Danagel yalijengwa mapema kutoka katika miamba kiasi cha miaka nusu milioni. Kama ilivyo kwa katika majengo mengine ya kifalme ya siku za Ufalme wa Aksum. Axum na Lalibela yamekuja tu kuhusishwa nayo baada ya vifo vyao. [11] kwa upande mwingine wanahistoria wa chini kama vile Getachew Mekonnen, anaunga mkono Masqal Kibra, malkia Lalibela kuwa alikuwa pia na moja ya makanisa (Abba Libanoa) ilijengwa kama kumbukumbu ya mume wake baada ya kifo chake.[12]
Tofauti na nadharia zilizoanzishwa na waandishi kama vile Graham Hancock mwamba mkubwa uliotokea na kuwa kanisa la Lalibela haukujengwa kwa msaada wa mfalme Knights Knights Templar: ushahidi mbalimbali umekuwa ukipatikana na kuonesha kuwa, kanisa hilo lilijengwa na watu wa kwanza kuwahi kuishi katika nchi ya Ethiopia.
Kama vile Buxton aliandika kuwa, lilivuta kuja kwa wageni wengi, kujenga kanisa hili na kuongeza kuwa, kuna kila dalili kuwa katika baadhi ya michoro, hutoa muungano na makanisa mengine kama vile makanisa ya Kiorthodoksi ya Mashariki ya Ethiopia na Kanisa la Kiorthodoksi la Misri), bado ana wasiwasi kuhusu asili halisi ya miundo hiyo, lakini wazo la hakika linabaki kuwa makanisa haya ya mawe yalifuata makanisa ya kale ambayo yenyewe bado yana mfumo na ushahidi wa mfumo wa asili ya Axum [13]
Makanisa haya bado yanatoa uhandisi wa ajabu, kuwa yana uhusiano na maji (ambayo yanapatikana katika chemchemi karibu na makanisa ya aina hiyo) na kukaribia kufanana na mfumo wa sayansi ya miamba ya artesians ambayo huleta maji juu ya milima ambapo ndipo mjii hupatikana.[14]
Picha
-
Bete Medhane Alem
-
Bete Amanuel
-
Ngoma za kiibada karibu na Bete Giyorgis
-
Bete Abba Libanos
-
Bete Maryam
Fasihi
Lalibela inatajwa kuwa mji wa mapadri wengi, makanisa ya miamba katika riwaya ya Tananarive Due, riwaya inayuhusisha udhanifu wa kisansi. My Soul to Keep.
Hancock, Graham, Carol Beckwith & Angela Fisher: African Ark - Peoples of the Horn, Chapter I: Prayers of Stone/The Christian Highlands: Lalibela and Axum, Harvill, An Imprint of HarperCollinsPublishers, ISBN 0-00-272780-3
Tazama pia
Marejeo
- ↑ CSA 2005 National Statistics Ilihifadhiwa 13 Agosti 2007 kwenye Wayback Machine., Table B.3
- ↑ Mwaka 1994, zoezi la uhesabuji watu liliweka kumbukumbu ya idadi ya watu kuwa 8,484 ambao kati yao 3,709 walikuwa wanaume na 4,775 walikuwa wanawake.
- ↑ "I weary of writing more about these buildings, because it seems to me that I shall not be believed if I write more ... I swear by God, in Whose power I am, that all I have written is the truth". Francisco Alvarez, The Prester John of the Indies yaliyotafsiriwa na C.F. Beckingham and G.W.B. Huntingford (Cambridge: Hakluyt Society, 1961), p. 226. Beckingham and Huntingford add an appendix which discuss Alvarez's description of these churches, pp. 526-42.
- ↑ De Castanhoso's account is translated in R.S. Whiteway, The Portuguese Expedition to Ethiopia (London: The Hakluyt Society, 1902), pp. 94-98.
- ↑ Sihab ad-Din Ahmad bin 'Abd al-Qader, Futuh al-Habasa: The conquest of Ethiopia, translated by Paul Lester Stenhouse with annotations by Richard Pankhurst (Hollywood: Tsehai, 2003), pp. 346f.
- ↑ Lakini Richard Pankhurst alielezea hofu yake juu ya tukio hilo, na kuelezea kuwa japokuwa Sihab ad-Din Ahman ya kanisa. (Lilikuwa limechongwa kutoka katika mlima lakini nguzo zake pia zilikuwa katika mlima. lakini ni kanisa moja tu, ndilo lililoandikwa. Pankhurst anongeza kuwa, “kitu cha pekee kuhusu Lalibela (kama kila mtalii anajua) ni kuwa sehemu ya miamba kama kumi na moja hivi.na si mmoja tu….na yapo katika jiwa moja likiwa limetupwa juu ya jiwe jingine” Pankhurst, "Did the Imam Reach Lalibela?" Addis Tribune, 21 Novemba 2003
- ↑ Pankhurst anaeleza kuwa, Royal Chronicles, ambayo imetajwa na Ahmad Gragn’s ilikuwa imetelekezwa katika katika wilaya kati ya mwezi wa saba na wa tisa mwaka 1531. Sihab ad-Din Ahmad, Futuh al-Hasasa, p. 346n. 785.
- ↑ Alimalizia kuwa, kuanzia Ahmad Gragn alipochoma kanisa katika Lalibela, ilikuwa karibu na Bete Medhane Alem. Na kama vikosi vya waislamu havikukosewa katika kuelekezwa basi ni dhahiri kuwa kanisa lililochomwa moto lilikuwa kanisa la Gannata Maryam, lililopo maili kumi 10, mashariki mwa Lalibela ambayo kama ilivyo kwa Lalibela , nguzo zake pia zimechongwa katika vilele vya mlima Sihab ad-Din Ahmad, Futuh al-Hasasa, p. 346n. 786.
- ↑ David Buxton, The Abyssinians (New York: Praeger, 1970), p. 110
- ↑ Buxton, The Abyssinians, p. 108
- ↑ "Medieval Houses of God, or Ancient Fortresses?" Archaeology (Novemba/Desemba 2004), p. 10.
- ↑ Getachew Mekonnen Hasen, Wollo, Yager Dibab (Addis Ababa: Nigd Matemiya Bet, 1992), p. 24.
- ↑ Buxton, The Abysssinians, pp. 103f
- ↑ Mark Jarzombek, “Lalibela and Libanos, the King and the Hydro-Engineer of the 13th Century,” Thresholds, pp. 78-82.
Soma zaidi
- David W. Phillipson, Ancient Churches of Ethiopia (New Haven: Yale University Press, 2009). Chapter 5, "Lalibela: Eastern Complex and Beta Giyorgis"; Chapter 6, "Lalibela: Northern Complex and Conclusions"
Viungo vya nje
- Ethiopian Treasures - Zagwe Dynasty, Rock-hewn Churches - Lalibela Ilihifadhiwa 25 Septemba 2008 kwenye Wayback Machine.
- Lalibela, a city carved from legend Ilihifadhiwa 12 Novemba 2006 kwenye Wayback Machine.
- www.imperialethiopia.org/history2.htm Ilihifadhiwa 5 Februari 2004 kwenye Wayback Machine.
- History of Lalibela churches Ilihifadhiwa 13 Desemba 2004 kwenye Wayback Machine.
- UNESCO World Heritage Site
- Lalibela site page in the Aluka digital library Archived 2012-07-17 at Archive.today
- Ethiopia - Timkat Celebration in Lalibela