Leopoldo III wa Austria

Mt. Leopoldo III alivyochorwa.

Leopoldo III wa Austria (kwa Kijerumani: Luitpold; maarufu tangu akiwa hai kama Leopoldo Mtawa; Melk, 1073 – Klosterneuburg, 15 Novemba 1136) alikuwa mfalme mdogo wa Austria tangu mwaka 1095 hadi kifo chake.

Anakumbukwa kwa kudumisha amani na kuleta maendeleo nchini na hasa kwa kujenga monasteri nyingi, pamoja na kupenda maskini na wakleri [1].

Mwaka 1125 alikataa kugombea cheo cha kaisari wa Ujerumani

Alitangazwa na Papa Inosenti VIII kuwa mtakatifu tarehe 6 Januari 1485.

Sikukuu yake ni tarehe 15 Novemba[2][3].

Angalia pia

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.