Malcolm Guthrie

Malcolm Guthrie (10 Februari 1903 - 22 Novemba 1972) alikuwa profesa wa Lugha za Bantu.

Anajulikana kwa uchambuzi wa Lugha za Kibantu katika makala ya Guthirie 1971, ambayo yamebaki makala muhimu hadi leo ingawa yamezeeka.

Maisha

Kuzaliwa

Malcolm alizaliwa Hove, Sussex, Uingereza.

Baba yake alikuwa ametokea Uskoti na mama yake Uholanzi.

Makala yake

Makala[1] yake ni Comparative Bantu[2] ambayo yalichapishwa katika matoleo manne:

  • Toleo la kwanza: mwaka wa 1967
  • Toleo la Pili: 1971
  • Toleo la Tatu na la Nne: 1970.

Matoleo haya yanatoa ainisho la jumla la Lugha za Bantu na pia kuyapa muundo mpya makala ya Proto Bantu kama Lugha itarajiwayo ya familia ya Kibantu.

Muundo wake mpya

Katika muundo wake mpya wa makala hiyo, Guthrie alitoa data kutoka 'Lugha 28 za majaribio' ambazo zilichaguliwa bila mpangilio maalumu.

Malalamiko yametolewa, kwa mfano na Möhlig[3], kwamba jambo hili linafanya makala yake kuwa ya kutotegemewa, kwa vile lugha zilizoundwa upya, na hivyo ukoo unaweza kuwa tofauti kutoka iwapo mmoja atabadilisha chaguo la lugha.

Guthrie pia alichapisha kwa ukubwa kuhusu lugha nyingi za Kibantu, ikiwemo Lingala, Baemba, Mfinu na Lugha ya Teke.

Tazama Pia

Virejeleo

  1. Guthrie, Malcolm (1948) The classification of the Bantu languages. London: Oxford University Press for the International African Institute.
  2. Guthrie, Malcolm (1967–71) Comparative Bantu: an introduction to the comparative linguistics and prehistory of the Bantu languages. 4 vols. Farnborough: Gregg Press.
  3. Möhlig, Wilhelm J.G. (1974) ‘Guthries Beitrag zur Bantuistik aus heutiger Sicht’, Anthropos, 71, 673-715.