Masimiani wa Bagai
Masimiani wa Bagai (alifariki 410 hivi) alikuwa askofu wa mji huo (leo nchini Algeria) aliyeteseka sana kwa ajili ya kupigania umoja wa Kanisa [1].
Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 3 Oktoba[2].
Maisha
Kwanza askofu wa madhehebu ya Wadonato, mwaka 401 alijiunga na Kanisa Katoliki na kuteswa sana kwa imani hiyo mpya, kiasi cha kuchukuliwa kama kielelezo cha ukali wa ushindani kati ya Wakristo wa Afrika Kaskazini. Mara mbili alinusurika kuuawa kwa mapigo ya Wadonato[3] hata Augustino wa Hippo alisema juu yake: Ana madonda mengi kuliko viungo.
Katika jaribio la kwanza alishambuliwa na umati ndani ya kanisa kuu,[4] akaokolewa na Wakatoliki baada ya kupata majeraha mengi.
Mara ya pili alishambuliwa na vikosi vya kijeshi vya Wadonato alipokwenda kutamalaki kikanisa kilichopiganiwa na pande hizo mbili hata mahakamani[5]. Alitupwa chini kutoka mnarani lakini aliangukia rundu la mboji. Hivyo hakufa walivyodhani maadui wake, bali alisaidiwa na wapitanjia akaendelea na juhudi zake.[6]
Mwaka 404 alimlalamikia kaisari Honori wa Dola la Roma[7], naye alirudisha hali ya kisheria dhidi ya Wadonato.[8]
Augustino katika barua ya mwaka 402 aliandika kuwa Masimiani alijiuzulu.[9] akamhimiza Kastori kushika nafasi ya ndugu yake ikawa hivyo.[10]
Tazama pia
- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
- ↑ https://www.santiebeati.it/dettaglio/72690
- ↑ Martyrologium Romanum
- ↑ Serge Lancel, Saint Augustine(Hymns Ancient and Modern Ltd, 2002)p289.
- ↑ Erika Hermanowicz, Possidius of Calama: A Study of the North African Episcopate in the Age of Augustine (Oxford University Press, 2008) p142.
- ↑ E. M. Atkins, Robert Dodaro, Augustine: Political Writings (Cambridge University Press, 2001) p241.
- ↑ J. Patout Burns, Robin M. Jensen, Christianity in Roman Africa: The Development of Its Practices and Beliefs (Wm. B. Eerdmans Publishing, 2014)p234.
- ↑ Erika Hermanowicz, Possidius of Calama: A Study of the North African Episcopate in the Age of Augustine [Oxford University Press|OUP Oxford], 2008) p149.
- ↑ Edward Ambrose Burgis, The annals of the Church [by E.A. Burgis p306.
- ↑ Nicene and Ante-Nicene Fathers, Ser. II, Vol. XIV.
- ↑ John E. Rotelle, The Works of Saint Augustine: A Translation for the 21st Century (New City Press, 2001 ) p262.
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |