Mbiu ya Pasaka

Shemasi akiimba mbiu ya Pasaka.

Mbiu ya Pasaka ni utenzi maalumu unaoimbwa na shemasi katika kesha la usiku wa Pasaka akiwa kwenye mimbari, karibu na mshumaa wa Pasaka.[1]

Utenzi huo ni maarufu kwa jina la Exsultet (yaani Ifurahi) kutokana na neno la kwanza katika lugha asili, ambayo ni Kilatini.

Kuna ushahidi wa uwepo wake mwishoni mwa karne ya 4.

Kutokana na uzuri wake, Wolfgang Mozart alisema: "Ningetoa miziki yote niliyoitunga kama ningeweza kuwa mtunzi wa Exsultet!"

Tanbihi

Viungo vya nje