Milki ya Bizanti
Ufalme wa Bizanti (kwa Kigiriki: Βυζαντινή Αυτοκρατορία) ni neno linalotumika kutaja Dola la Roma lilivyoendelea mashariki mwa eneo la kandokando ya bahari ya Mediteranea katika Zama za Kati, ukiwa na makao yake makuu kwenye mji wa Konstantinopoli (ulioitwa pia Bizanti) na kutumia lugha ya Kigiriki.
Katika baadhi ya maana, hasa baada ya kuanguka kwa Dola la Roma Magharibi na mjini Roma penyewe, hujulikana pia kama Dola la Roma Mashariki.
Wabizanti wenyewe walijiona ni bado Dola la Roma likiendelea tu. Watawala walitumia cheo cha "Kaisari" kama awali.
Hata hivyo, kwa wakati mwingi wa historia yake, ulifahamika na wenzao wa Ulaya magharibi kama “Ufalme wa Wagiriki” au “Ufalme wa Konstantinopoli” au "Rhômania".
Lakini majirani wa mashariki kama Waarabu waliendela kuwaita "Waroma" (kwa Kiarabu روم rum).
Bizanti ilipata mapigo mawili makubwa katika historia yake:
- Uvamizi wa Waarabu Waislamu kuanzia mwaka 636 uliosababisha kupotea kwa majimbo ya Afrika ya Kaskazini, Misri na Shamu
- Uvamizi wa jeshi la Wakristo la Vita vya msalaba walioteka mji wa Konstantinopoli mwaka 1204. Shambulio hili lilisababisha nguvu za ufalme kufifia kabisa. Hata baada ya watawala wa Bizanti kurudi Konstantinopoli walikosa nguvu ya kujihami dhidi ya Waturuki Waosmani. Hatimaye hao waliteka Konstantinopoli mwaka 1453 na kumaliza kabisa Bizanti uliokuwa umetunza urithi wa Roma ya Kale hadi wakati ule.
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Ufalme wa Bizanti kama enzi zake au matokeo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |