Mkarakara

Mkarakara
(Passiflora spp.)
Mkarakara-jeusi
Mkarakara-jeusi
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Plantae (Mimea)
(bila tabaka): Angiospermae (Mimea inayotoa maua)
(bila tabaka): Eudicots (Mimea ambayo mche wao una majani mawili)
(bila tabaka): Rosids (Mimea kama mwaridi)
Oda: Malpighiales (Mimea kama mwenda-usiku
Familia: Passifloraceae (Mimea iliyo mnasaba na mkarakara)
Jenasi: Passiflora
L.
Ngazi za chini

Spishi >500; 4 zinakuzwa katika Afrika ya Mashariki:

  • P. edulis Sims
  • P. ligularis Juss.
  • P. quadrangularis L.
  • P. tarminiana Coppens & V.E.Barney au P. tripartita (Juss.) Poir.

Mikarakara au mipesheni ni mimea mitambazi ya jenasi Passiflora katika familia Passifloraceae. Matunda yake huitwa makarakara au mapesheni. Kuna takribani spishi 550.

Asili ya mimea hiyo ni Amerika, ya Kati na ya Kusini hasa. Siku hizi spishi kadhaa hukuzwa sana katika ukanda wa tropiki, na katika Afrika ya Mashariki mkarakara-jeusi na mkarakara-tamu na mkarakara-njano inajulikana sana tangu mwanzo mwa karne ya 21.

Spishi zinazokuzwa katika Afrika ya Mashariki

  • Passiflora edulis
    • P. edulis forma edulis Mkarakara-jeusi
    • P. edulis forma flavicarpa Mkarakara-njano
  • Passiflora ligularis Mkarakara-tamu
  • Passiflora quadrangularis Mkarakara-kubwa
  • Passiflora tarminiana au Passiflora tripartita var. mollissima (uainishaji umechanganyika) Mkarakara-ndizi

Picha

Marejeo

Makala hii kuhusu mmea fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkarakara kama uainishaji wake wa kibiolojia, uenezi au matumizi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.