Mpango wa Biashara
Mpango wa biashara ni kauli rasmi ya malengo ya biashara, sababu zinazoyafanya yakisiwe kuwa yanawezekana, na mpango wa kutimiza malengo hayo. Aidha inaweza kuwa na habari msingi kuhusu shirika au kundi linalojaribu kufikia malengo hayo.
Malengo ya biashara yanaweza kufafanuliwa kwa mashirika ambayo lengo lao ni faida na yale yasiyo ya faida. Mpango wa biashara za mashirika ya faida kimsingi husistiza malengo ya kifedha, kama vile faida ama kupata mali. Ramani za biashara za mashiirka yasiyo ya faida na yale ya serikali husisitiza zaidi kwenye azma ya shirika hilo ambayo ndiyo nguzo ya serikali ama hali yao ya kutotaka faida ama kutotoza ushuru kwa usanjari huo- ingawa mashirika yasiyo ya faida yanaweza pia kuzingatia mapato. Katika mashirika yasiyo ya faida, matatizo hutokea wakati kuna juhudi za kusawazisha lengo na "tofauti za faida" (au mapato). Mipango ya biashara inaweza kuwa inalenga mabadiliko ya mitazamo na utambulisho wa wanunuzi, wateja, walipa kodi ama jamii kwa ujumla. Mpango wa kibiashara wenye mabadiliko katika mitazamo na utambulisho kama malengo yake makuu unaitwa mpango wa soko.
Hadhira
Mpango wa biashara unaweza kulenga ndani ama nje ya shirika. Mipango inayolenga nje hukusudiwa malengo ambayo ni muhimu kwa washikadau wa nje, hususan wale wa kifedha. Wana habari za kina kuhusu shirika ama kundi linalojaribu kufikia malengo hayo. Kwa mashirika ya faida, washikadau wa nje ni pamoja na wawekezaji na wateja. [1] Washikadau wa mashirika yasiyo ya faida ni pamoja na wafadhili na wateja wa huduma zisizo za faida. [2] Kwa upande wa mashirika ya serikali, washikadau wa nje ni pamoja na walipa kodi, mashirika ya serikali ya ngazi za juu, na mashirika ya kimataifa ya mikopo kama vile Shirika la Fedha Duniani, Benki ya Dunia, mashirika mbalimbali ya kiuchumi ya Umoja wa Mataifa, na benki za maendeleo.
Mipango ya biashara ya ndani hukusudiwa malengo ya kati ambayo yanahitajika ili kufikia malengo ya nje. Mipango hiyo inaweza kujumuisha uanzishaji wa bidhaa mpya, huduma mpya, mfumo mpya wa kiteknolojia, kupanga upya fedha, kurekebisha kiwanda ama kuratibu upya shirika. Mpango wa biashara wa ndani aghalabu hukuzwa pamoja ma kadi iliyo na orodha ya mambo ambayo yatawezesha mafanikio. Hii huwezesha mafanikio ya mpango kupimwa kwa kutumia njia zisizo za kifedha Mpango wa biashara ambao hubaini na kusisitiza malengo ya ndani, lakini unatoa mwongozo wa kijumla tu wa jinsi yatafikiwa huitwa mkakati.
Mipango tekelezi hueleza malengo ya ndani ya shirika, kundi la kazi au idara. [3] Mipango ya miradi, amabayo pia huitwa mifumo ya miradi, huelezea malengo ya mradi mahususi. Aidha, inaweza kushughulikia nafasi ya muradi katika mkakati mzima wa shirika. [4] [5]
Yaliyomo kwenye Mpango wa Biashara
Mpango wa biashara ni vifaa vya kufanyia uamuzi. Hakuna mambo maalum yanayounda mpango wa biashara: hii ni kwa sababu mipango ya biashara hutofautiana. Kwa kiasi fulani, muundo na yaliyomo kwenye mpango wa biashara hutokana na malengo pamoja na hadhira. Ni sharti mpango wa biashara ijumuishe kila habari inayohitajika kuamua kutekeleza lengo fulani.
Kwa mfano, mpango wa biashara wa shirika lislo la kifaida hufafanua ukubalifu kati ya mpango wa biashara na malengo ya shirika hilo. Mara nyingi hofu ya benki huwa ni makosa, hivyo mpango wa biashara wa kutafuta mkopo wa benki utashawishi kuhusu uwezo wa wa shirika kulipa mkopo huo. Kimsingi wawekezaji wa mtaji hujihusisha na uwekezaji wa awali, uwezekano wa kufaulu na kutathmini jinsi ya kutamatisha. Mpango wa biashara wa mradi unaohitaji fedha utahitaji kueleza kwa nini rasilimali zilizopo kwa sasa, nafasi za biashara zinazoibuka, na faida ya ushindani endelevu itawaletea ufanisi mwishoni.
Utayarishaji wa mpango wa biashara huhitaji maarifa kutoka kwa taaluma za biashara mbalimbali: fedha, na usimamizi wa wafanyakazi, usimamizi wa ujuzi-nafsi, usimamizi wa ugavi, usimamizi wa shughuli, na masoko, miongoni mwa mengine. Ni jambo muhimu kuangalia mpango wa biashara kama mkusanyiko wa mipango midogomidogo, moja kwa kila taaluma kuu ya biashara. [6]
"... mpango wa biashara mzuri unaweza kusaidia kufanya biashara nzuri iwe ya kuaminika, ya kueleweka, na kuvutia kwa mtu ambaye hana ufahamu wa biashara hiyo. Uandishi mpango mzuri wa biashara haumaanishi kuwa utafaulu, lakini unaweza kusaidia katika kupunguza uwezekano wa kutofanikiwa. " [6]
Miundo ya uwasilishaji
Muundo wa muundo wa biashara hutegemea muktadha wake wa kuwasilisha. Si nadra kwa mashirika ya biashara, hasa yale yamayoanza, kuwa na miundo mitatu au minne ya mpango wa biashara:
- "kiwango kilichokuzwa" - ni muhtasari wa dakika tatu wa ufupisho wa mpango tendaji wa biashara. Mara nyingi hii hutumika kama kichocheo kuamsha hisia za wanaotarajiwa kuwa watafadhili, wanunuzi ama washirika muhimu.
- Uwasilishi wa masimulizi- mawasilisho ya slaidi pamoja na masimulizi ya kufurahisha ambayo yameazimiwa kuanzisha majadiliano na kuwapa hamu wawekezaji watarajiwa kusoma wasilisho la mchapisho. Mara nyingi maudhui ya uwasilishaji hutegemea muhtasari wa utendaji na michoro michache ya kimsingi inayoonyesha hali za kifedha na vigezo muhimu vya maamuzi. Iwapo bidhaa mpya inapendekezwa na muda upo, maonyesho ya bidhaa hiyo yanaweza kujumuishwa.
- Kuwe na wasilisho la maandishi kwa washikadau wa nje - lililo na habari za kutosha, na lililopangwa vizuri kwa ajili ya washikadau wa nje.
- Mpango wa biashara wa ndani- mpango wenye maelezo ya kutosha yanayohitajika na usimamizi lakini huenda yasiwe ya muhimu kwa washikadau wa nje. Mipango kama hiyo huwa na uwezo wa aina fulani wa kuweka habari wazi na kufahamisha kuliko muundo ambao hulengwa kwa washikadau wa nje.
Mfano wa muundo wa mpango wa biashara wa kuanzisha mradi [7]
- jalada na yaliyomo
- muhtasari tendaji
- maelezo ya biashara
- uchambuzi wa mandhari ya biashara
- maelezo msingi ya biashara
- uchambuzi wa ushindani
- uchambuzi wa soko
- mipango ya uuzaji
- muundo wa utekelezaji
- muhtasari wa usimamizi
- utaratibu wa fedha
- viambatisho na mambo muhimu
Kuangalia tena Mpango wa Biashara
Gharama na nakisi ya mapato
Makadirio ya gharama na mapato ni muhimu katika mpango wo wote wa biashara ili kufanya uamuzi kuhusu uwezekano wa biashara unaonuiwa kuanzishwa. Hata hivyo, mara nyingi gharama huwa inapunguzwa na mapato kuongezwa hivyo basi baadaye husababisha nakisi ya mapato na huenda biashara inaishilia kutolipa. Wakati wa bubujiko la mtandao, 1997-2001 hili lilikuwa tatizo kwa wengi waliokuwa wanatangamana na teknolojia kwa mara ya kwanza. Hata hivyo, tatizo hili si la teknolojia au sekta binafsi pekee; miradi ya umma kwa kawaida huathiriwa na kuongezeka kwa gharama na /au nakisi ya mapato pia. Sababu za kuongezeka gharama na nakisi ya mapato ni matumaini ya kupendelea kukosa kufasiri mikakati ipasavyo. [8] [9] Kiwango cha marejeo cha kukadiria kimebuniwa ili kupunguza uwezekano wa kuwa na kuongezeka kwa gharama na nakisi ya mapato.
Masuala ya Kisheria na Vikwazo
Mahitaji ya kufichua
Lazima mpango wa biashara unaolenga nje uorodheshe mambo yote ya kisheria na vikwazo vya fedha ambavyo vinaweza kuathiri vibaya wawekezaji. Kutegemeana kiasi cha fedha zinazotafutwa na hadhira ambayo mpango huu unawasilishwa, kukosa kufanya hivyo kutasababisha madhara kadhaa ya kisheria.
Upungufu wa yaliyomo na hadhira
Mikataba ya kutoweka wazi (NDAs) na wahusika wasio wanachama, makubaliano dhidi ya ushindani, migogoro nia, haki ya kutoingiliwa, na ulinzi wa siri za biashara huweza kupunguza hadhira ambayo mtu anaweza kuonyesha mpango wa biashara. Aidha, wanaweza kutaka kila upande unaopokea mpango wa biashara kutia sahihi kandarasi ya kukubali masharti na vipemgele muhimu.
Hali hii huwa na utata kutokana na ukweli kwamba wawekezaji wengi wa mtaji watakataa kutia sahihi mkataba wa kutoweka wazi (NDA) kabla ya kuuona mpango wa biashara, la sivyo utawaweka katika hali isiyofaa ya kuangalia mipango biashara miwili inayofanana, kila moja ikidai ndiyo ya kwanza kuandikwa. Katika hali kama hiyo mtu atahitjika kutenegeneza mipango miwili ya biashara: moja isiyo na maelezo mengi ambayo inaweza kutumika kuanzisha uhusiano na ruwaza yenye maelezo mengi ambayo huonyeshwa wawekezaji baada ya wao kuwa nia ya kuridhisha na imani ya kutia sahihi mkataba wa NDA.
Mipango ya Biashara Wazi
Kwa kawaida, mipango ya biashara imekuwa ya siri na huwa na hadhira ndogo. Mpango wa biashara wenyewe huchukuliwa kama siri. Hata hivyo, kuibuka kwa programu na chanzo huru kumekiweka wazi kielelezo hiki na kufanya dhana ya biashara wazi iwezekane.
Mpango wa biashara wazi ni mpango wa biashara ulio na hadhira pana. Kwa kawaida, mpango wa biashara hii huchapishwa kwenye tovuti ili isomwe na kila mtu.
Kwenye kielelzo cha programu huru na biashara ya chanzo huru, siri za biashara, hakimiliki na hataza haziwezi kutumika kama mikakati mwafaka ya kufunga ili kutoa manufaa ya kudumu kwa biashara mahususi kwa hivyo, mpango wa biashara haufai sana kwa vielelezo hivi.
Huku asili ya mpango wa biashara huru ukiwa kwenye programu huru na huduma za eneo la Libre, dhana hiyo inaweza kutumika kwenye nyanja zingine.
Jinsi Mipango ya Biashara inavyotumika
Mtaji wa uwekazaji
- mashindano ya mipango ya biashara - hutoa mwelekeo wa mtaji kupata miradi yenye matumaini
- makadirio ya mtaji wa uwekezaji wa mpango wa biashara - huzingatia maswala ya ubora kama vile ya kundi.
Mchango wa Umma
- katika mchango wa umma, wawekezaji watarajiwa wanaweza kutathmini mitazamo ya kampuni
Ndani ya Mashirika
Kuchangisha pesa
Lengo la msingi la mpango wa biashara nyingi ni kuchangisha pesa, kwa sababu kuna uhusiano wa moja kwa moja na hatari ya kufanikiwa ama kuangka kwa kampuni.
Jumla ya Usimamizi Mzuri
Jumla ya Usimamizi Mzuri (TQM) ni mkakati wa usimamizi wa biashara wenye lengo la kuhamasisha kuhusu ubora katika michakato yote ya shirika. Jumla ya Usimamizi Mzuri umetumika katika uzalishaji, elimu, vituo vya kupiga simu, serikali, mashirika ya huduma, kadhalika shirika la anga la NASA na miradi ya sayansi.
Usimamizi kupitia kwa Malengo
Usimamizi kupitia kwa Malengo (MBO) ni mchakato wa kukubaliana kuhusu malengo katika shirika ili uongozi na wafanyakazi wakubaliane kuhusu malengo na kuelewa nafasi yao kwenye shirika hilo.
Kuweka Mikakati
Kupanga Mkakati ni utaratibu wa kampuni kuelezea mkakati wake, ama mwongozo na kufanya maamuzi jinsi ya kugawa rasilimali yake ili kufikia mkakati huo, ikiwa ni pamoja na mtaji na watu. Mbinu mbalimbali za kuchambua biashara zinaweza kutumika kwenye mkakati wa mpango, pamoja na uchanganuzi wa UUFC (Uwezo, Udhaifu, Fursa, na Changamoto) na uchambuzi wa SUJT (Kisiasa, Kiuchumi, Kijamii, na Kiteknolojia) au uchambuzi JTUMD uchambuzi unaoshirikisha Tamaduni-Jamii, Teknolojia, Uchumi, Ikoloji, Udhibiti wa vipengele vya mabadiliko na MSEJTUSR (Mazingira, Siasa, Enye kuelimisha, Kijamii, Kiteknolojia, Kiuchumi, Kisheria na Kiroho)
Elimu
K-12
Mpango wa biashara hutumiwa katika baadhi ya vipindi vya shule za msingi na upili kufundishia kanuni za kiuchumi. [10] Wikiversity ina mradi wa Lunar Boom Town ambapo wanafunzi wa umri wote wanaweza kushirikiana na kubuni na kurekebisha mifumo ya biashara na kufanya mazoezi ya kuitathmini ili kujifunza katika hali ya kiutendaji mbinu na njia za kuratibu biashara.
Elimu ya Juu
- Shahada za BA na MBA.
- miradi inayojumuisha makundi
- miradi ya kozi maalumu
- Mashindano ya mipango wa biashara
Uhakiki wa Mipango ya Biashara
Mpango wa biashara huwa na namna nyingi za kuhakikiwa. Uhakiki hutumiwa kuitweza mipango ya biashara na pia kama chombo cha kuelimisha ili kukoleza ubora wa mpango wa biashara. Kwa mfano,
- Hatua tano za kufanikiwa kwa mpango wa biashara katika bayoteknolojia Ilihifadhiwa 6 Januari 2012 kwenye Wayback Machine. hutumia michoro ya kuchekesha ya Dilbert kuwakumbusha watu kile wasichopaswa kufanya wakati wa kufanya utafiti wa kuandika mpango wa biashara za kuanza mradi wa kibayoteki. Mwandishi wa kitabu cha Dilbert, Scott Adams, aliye na shahada ya uzamili ya MBA (U.C. Berkeley), anaona ucheshi kama chombo muhimu ambacho kinaweza kuboresha tabia za mameneja na biashara. [11] Ameandika hakiki nyingi za shughuli za biashara ikiwa ni pamoja na kupanga biashara. Tovuti ya Dilbert.com - Games Ilihifadhiwa 17 Desemba 2009 kwenye Wayback Machine. ina kifaa cha kauli mbiu ambacho huhakiki maneno yanayopatikana katika kauli mbiu. Kitabu chake "The Dilbert Principle - A Cubicle's Eye View of Bosses, Meetings, Management Fads & Other Workplace Afflictions" kinajadili makosa madogomadogo ya usimamizi na mipango yake kama inavyojidhihirisha kwenye michoro ya uchekeshaji ya Dilbert na Scott Adams.
- Kwenye makala "South Park's" Investing Lesson, katika The Motley Fool "Fool on the Hill", mwandishi anatumia Chupi za Kizimwi kuonyesha makosa ya kusisitiza malengo bila ya utekelezaji mzuri wa mkakati. Kisa cha Chupi za Kizimwi kinahakiki mpango wa biashara wa kipindi cha sasa.
Marejeo
- ↑ Maelezo ya biashara ndogo Ilihifadhiwa 26 Novemba 2010 kwenye Wayback Machine.muongozo wa mpango wa biashara wa kuanzisha biashara ndogondogo
- ↑ Kituo cha Ubora bila Faida Ilihifadhiwa 13 Mei 2008 kwenye Wayback Machine. mpango wa biashara usio kwa ajili ya faida
- ↑ Jimbo la Louisiana, USA Ilihifadhiwa 7 Machi 2007 kwenye Wayback Machine. mpango wa uendeshaji shirika la serikali
- ↑ Visitask Ilihifadhiwa 11 Januari 2010 kwenye Wayback Machine. mpango wa mradi
- ↑ Mradi wa serikali ya Tasmanian kuhusu usimamizi msingi wa elimu Ilihifadhiwa 22 Juni 2009 kwenye Wayback Machine. mpango wa mradi wa serikali
- ↑ 6.0 6.1 Eric S. siegel, Brian R. Ford, Jay M. Bornstein (1993), 'The Ernst & Young Business Plan Guide' (New York: John Wiley na Wana) ISBN 0471578266
- ↑ Harvard Business School Press-Pocket Mentor, "Creating a Business Plan"
- ↑ Bent Flyvbjerg, Mette K. Holm Skamris, na Søren Yale Buhl (2002), "Underestimating Costs in Public Works Projects: Error au Lie?" Ilihifadhiwa 25 Mei 2012 kwenye Wayback Machine. Journal of the American Association, vol. 68, no. 3, 279-295.
- ↑ Bent Flyvbjerg, Mette K. Holm Skamris, na Søren Yale Buhl (2005), "How (Katika)accurate Are Demand Forecasts in Public Works Projects?" Ilihifadhiwa 5 Februari 2012 kwenye Wayback Machine. Journal wa Mipango wa Marekani Association ayaa waxaa sidoo kale, Juz. 71 hakuna. 2, 131-146.
- ↑ [14] ^ Pennsylvania Business Plan Competition Ilihifadhiwa 18 Machi 2016 kwenye Wayback Machine. - shindano lililolenga kufundisha kanuni za kiuchumi kwa wanafunzi wa K-12
- ↑ "Tricia Bisoux, "Funny Business", BizEd, Novemba / Desemba, 2002" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2010-05-28. Iliwekwa mnamo 2009-12-15.