Mto Saint Lawrence

Mto Saint Lawrence
Mto Saint Lawrence mjini Montreal
Chanzo Ziwa Ontario, 44°06′N 76°24′W / 44.100°N 76.400°W / 44.100; -76.400
Mdomo Ghuba ya Saint Lawrence, Atlantiki
Nchi Kanada, Marekani
Urefu km 500
Mkondo 16,800 m3/s
Miji mikubwa kando lake Montreal, Quebec

Mto Saint Lawrence (kwa Kiingereza: Saint Lawrence River, kwa Kifaransa: Fleuve Saint-Laurent) ni mto mkubwa katika Amerika ya Kaskazini. Mwanzoni unafuata mpaka baina ya Kanada na Marekani halafu unapita katika jimbo la Quebec hadi kuishia katika Ghuba ya Saint Lawrence na Bahari Atlantiki.

Chanzo chake kipo pale unapoondoka katika Ziwa Ontario. Lakini ilhali maziwa makubwa ya Amerika Kaskazini yote yameunganika, maji ya maziwa hayo yote huelekea baharini kupitia mto Saint Lawrence. Kwa hiyo inawezekana kuhesabu vyanzo vyote vya maziwa hayo kuwa vyanzo vya mto Saint Lawrence, na kwa mtazamo huu urefu wake ni zaidi ya kilomita 3,000.

Mdomo wake ni mpana sana na huitwa Ghuba ya Saint Lawrence. Umbali baina ya Ziwa Ontario na Ghuba ya Saint Lawrence ni kilomita 500.

Upande wa Kanada kuna miji ya Kingston, Montreal, Trois-Rivières na Quebec City kando ya mto huu. Meli kubwa zinaweza kuutumia kama njia baina ya Maziwa Makuu na Atlantiki.

Tanbihi

Viungo vya Nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu maeneo ya Kanada bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mto Saint Lawrence kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.