Mwambatope
Mwambatope (kwa Kiingereza: shale rock) ni aina ya mwamba mashapo yenye chembe ndogo sana; asili yake ni mashapo ya matope.
Matope yanayofanya mwambatope ni ya udongo wa mfinyanzi (clay) pamoja na chembe ndogo za kwatzi na kalsiti.[1]
Mara nyingi mwambatope yanatokea kwa matabaka membamba yanayoweza kutenganishwa kirahisi. Kama aina hii ya mwambatope inaathiriwa na shinikizo na joto kubwa zaidi itakuwa mwamba metamofia aina ya grife unaovunjika kwa urahisi kwa bapa nyembamba kama sahani yaani sleti. Hizo zinatumiwa kama bapa za kuezeka mapaa ya nyumba.
Kutokea kwa mwambatope
Matope yatakayounda mwambatope hukusanyika katika maji yenye mwendo wa polepole au pale ambapo mito inaishia ziwani, katika delta ya mto au katika vilindi vya baharini pasipo mikondo ya bahari. Mchakato wa kukusanyika na kuwa mwamba unachukua mamilioni ya miaka.
Marejeo
- ↑ Blatt, Harvey and Robert J. Tracy 1996. Petrology: igneous, sedimentary and metamorphic. 2nd ed, Freeman, 281 - 292
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mwambatope kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |