Mwenge

Kwa maana tofauti ya jina hili angalia hapa Mwenge (maana)

Maandamano ya usiku nchini Uingereza, watu hubeba mienge

Mwenge (pia: tochi[1]) ni kifaa cha kubebea moto kwa kusudi la kuangaza mazingira.

Kwa kawaida ni fimbo lenye sehemu ya kuwaka upande mmoja; sehemu hii inapatikana kwa kupaka mafuta upande mmoja wa fimbo, au kuifunika kwa nta, au kuiviringisha kwa kitambaa chenye mafuta ndani yake. Mienge ya kisasa hutumia pia mafuta, gesi au kemikali mbalimbali.

Katika historia pasipo na taa za mafuta zinazoweza kubebwa na kabla ya kupatikana kwa umeme miengi ilitumiwa kuangaza njia gizani au pia nyumba.

Katika kipindi cha zama za mwangaza mwenge ulitumiwa kama ishara ya mwangaza unaosambaza nuru ya akili na falsafa kwenye giza ya ujinga na ushirikina. Kwa maana hii Sanamu ya Uhuru huko New York inashika mwenge.

Siku hizi mienge hutumiwa

  • kwa burudani, pale ambako watu hutaka kuwa na angaza kwa muda tu au wakiona miembe ni njia ya kupamba bustani wakati wa sherehe
  • katika hali ya dharura, kwa mfano wapanda mlima hubeba mienge ya rangi kama alama ya kuomba msaada, au askari wana akiba ya miembe kama tahadhari kama taa za umeme zinakwama
  • kwa sherehe maalum, kwa mfano miembe ya kubeba moto ya Michezo ya Olimpiki kutoka Olimpia hadi mahali pa michezo; pia Mwenge wa Uhuru ambao ni ishara ya kitaifa nchini Tanzania.

Maelezo

  1. "Tochi" hutumiwa pia kutaja taa ya mkononi inayotumia umeme wa beteri