Nyaraka za Kichungaji
Nyaraka za Kichungaji ni kundi la maandiko ya Agano Jipya katika Biblia ya Kikristo. Jina hilo linajumlisha barua moja kwa Tito na mbili kwa Timotheo, ambao walikuwa washiriki wakuu wa kazi ya Mtume Paulo, wakawa waandamizi wake.
Wataalamu wanabishana sana kuhusu mtunzi wa barua hizo, wengi wakidhani zimeandikwa na mfuasi wa Paulo mwaka 95 hivi, huku wengine wakishikilia aliziandika mwenyewe, kwa msaada wa karani fulani, miaka ya mwisho ya maisha yake (63-67), ambapo baada ya kufunguliwa aliweza kusafiri tena mashariki (Ugiriki na nchi za kandokando) na pengine hata magharibi (Hispania).
Waraka wa pili kwa Timotheo unaonekana kama wasia wake aliouandika kifungoni akisubiri kuuawa.
Barua hizo zinaitwa za kichungaji kwa kuwa ziliandikwa kwa maaskofu hao ili kuwasaidia kufanya vizuri kazi zao, hasa kwa kushika imani sahihi, kupinga uzushi, kuchagua vizuri viongozi ambao wawawekee mikono, kuchunga vema Wakristo wa aina mbalimbali, kuwa na mwongozo kuhusu ibada, n.k.
Ndiyo sababu ni muhimu sana kwa miundo ya Kanisa iliyokuwa mbioni kupata sura yake ya kudumu.
Pamoja na hayo zinahimiza kukubali mateso kwa ajili ya Injili: ndio msimamo wa Mchungaji mwema (Tito 1:5-9; 2; 1Tim 1:18-2:10; 3:1-4:16; 6:2b-21; 2Tim. 1:3-14; 2:1-18; 3:14-17; 4:1-8).
Viungo vya nje
- Calvin, John (1556 [1-2 Tim]; 1549 [Titus]). Commentary on 1-2 Timothy and Titus.
- PastoralEpistles.com Ilihifadhiwa 20 Oktoba 2021 kwenye Wayback Machine., an academic blog devoted to current research in the letters:
- Bumgardner, Charles (2016). "Paul's Letters to Timothy and Titus: A Literature Review (2009-2015)" Ilihifadhiwa 9 Septemba 2021 kwenye Wayback Machine.
- Klinker-De Klerck, Myriam (2008). "The Pastoral Epistles: Authentic Pauline Writings"
- Early Christian Writings:
- Pastoral Epistles
Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Nyaraka za Kichungaji kama historia yake au athari wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |