Nyigu-mende

Nyigu-mende
Nyigu-johari (Ampulex compressa)
Nyigu-johari (Ampulex compressa)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye miguu yenye viungo)
Nusufaila: Hexapoda (Wanyama wenye miguu sita)
Ngeli: Insecta (Wadudu)
Ngeli ya chini: Pterygota (Wadudu wenye mabawa)
Oda: Hymenoptera (Wadudu wenye mabawa mangavu)
Nusuoda: Apocrita (Hymenoptera wenye kiuno chembamba)
Familia ya juu: Apoidea
Familia: Ampulicidae
Shuckard, 1840
Ngazi za chini

Nusufamilia 2:

  • Ampulicinae Shuckard, 1840
  • Dolichurinae Lepeletier, 1845

Nyigu-mende (kutoka kwa Kiing. cockroach wasps) ni nyigu wadogo wa familia Ampulicidae katika familia ya juu Apoidea ya oda Hymenoptera ambao huwapatia mabuu wao mende kama chakula. Spishi zilizo na rangi zing'aazo huitwa nyigu-johari.

Maelezo

Hawa ni nyigu wadogo wenye urefu wa mm 4-14, madume wakiwa wadogo kuliko majike. Fumbatio ni fupi na siyo ndefu kuliko thoraksi. Sehemu za mdomo ni ndefu. Nyuma ya kichwa kuna “shingo” na pamoja na mifuo ya thoraksi na kiuno chembamba sana wanafanana na sisimizi, haswa spishi nyeusi. Nyingi nyingine zina rangi zing'aazo kama kijani, buluu au nyekundu.

Biolojia

Nyigu-johari akivuta mende aliyewekwa kitulizo na nyigu huyu.

Nyigu hawa ni vidusia wa mende, kila spishi ikibobea katika spishi moja au kadhaa za mende. Mende aliyebumbuazwa huingizwa kwenye shimo la kiota ambalo hutokea kiasili kwenye tawi, mwamba au ardhi. Kisha yai hutagwa juu ya mbuawa na shimo limefungwa na takataka. Maelezo yafuatayo ya mchakato huo huchukua Ampulex compressa kama mfano[1].

Nyigu jike humvamia mende kwa kumchoma haraka kwenye ganglioni la thoraksi ili kumpoozesha kwa muda. Baadaye, ana nafasi ya kutosha ya kutumia mchomo wa usahihi katika sehemu ya ubongo ambayo inawajibika kwa sihiari ya kukimbia. Kwa hivyo, mende anapopona kutokana na kuchomwa kwa mara ya kwanza, amechanganyikiwa na kujiruhusu kuvutwa kwenye shimo la kiota akiwa bado anatembea peke yake. Hii inaruhusu nyigu kutumia mbuawa mkubwa ambayo vingenevyo angekuwa mzito sana kubebwa. Ndani ya kiota hutaga yai kwenye moja ya koksa za katikati za mende. Buu anayeibuka hula kwenye mbuawa aliye bado hai na huwa bundo ndani yake. Nyigu hatimaye huibuka na kuacha shimo la kiota.

Spishi za Afrika ya Mashariki

  • Ampulex compressa, Nyigu-johari
  • Ampulex kristenseni
  • Ampulex melanocera
  • Ampulex nasuta
  • Ampulex nitidicollis
  • Ampulex toroensis
  • Dolichurus ignitus

Picha

Marejeo