Olaf Scholz
Olaf Scholz (amezaliwa Osnabrück, 14 Juni 1958) ni mwanasiasa wa Ujerumani aliyechaguliwa Chansela wa Ujerumani tarehe 8 Desemba 2021.
Scholz ni mwanachama wa Chama cha Kijamaa-Kidemokrasia cha Ujerumani (SPD) akiongoza serikali ya ushirikiano na Chama cha Kijani na chama cha Liberali FDP.
Kabla ya kuchaguliwa kuwa chansela alikuwa makamu wa Angela Merkel na waziri wa fedha katika serikali ya ushirikiano wa CDU na SPD kuanzia 2018 hadi 2021.
2011 hadi 2018 alikuwa waziri mkuu wa jimbo la Hamburg.
Scholz alisoma sheria alikuwa wakili. Alijunga na chama cha SPD mnamo 1970 akaingia kwenye bunge la kitaifa mara ya kwanza mnamo mwaka 1998. Mwaka 2002 aliteuliwa kuwa katibu mkuu wa SPD. Katika serikali ya kwanza ya Merkel alikuwa waziri wa kazi tangu 2007 hadi kurudi katika siasa ya jimbo la Hamburg.
Viungo vya nje
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Olaf Scholz kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |