Orodha ya departements za Ufaransa

Departement ni kitengo cha utawala nchini Ufaransa. Inalingana na ngazi ya wilaya. Departement inaongozwa na mkuu wake ambaye kwa lugha ya Kifaransa anaitwa prefect.

Kwa jumla kuna wilaya 101 za aina hii. Hizi zimepangwa katika mikoa (region) 18.

Kati yake, departement 96 tu ziko Ufaransa bara na kisiwa jirani cha Corsica, nyingine 5 ziko nje ya Ulaya ambako wakazi wa yaliyokuwa makoloni waliamua kubaki sehemu za Ufaransa na maeneo hayo kupewa hadhi ya departement, wakati huohuo ni pia mikoa. Hizi departments za ng'ambo ni: Guadeloupe na Martinique katika Karibi, Guayana katika Amerika Kusini, Réunion na Mayotte) kwenye bahari Hindi.

Historia

Baada ya mapinduzi ya mwaka 1789 Ufaransa yote iligawiwa katika wilaya (kwa Kifaransa "département") zilizoongozwa na mkuu (prefect) aliyekuwa mwakilishi wa serikali kuu.

Tangu mwaka 1964 wilaya ziliwekwa chini ya ngazi mpya ya mikoa ("région").

Tangu mwaka 1982 Ufaransa ilianza kutumia mfumo wa ugatuzi na kuipa mikoa, wilaya na kata zake kiwango cha madaraka ya kujitawala. Tangu hapo kila department imepata halmashauri yake inayochaguliwa na raia wa eneo lake.

Orodha

Mikoa na departements za Ufaransa:

Makala hii kuhusu maeneo ya Ufaransa bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Orodha ya departements za Ufaransa kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.