Poto au koni ni wanyama wadogo wa nusufamiliaPerodicticinae katika familia Lorisidae. Wamo miongoni mwa wanyama wa asili wa jamaa ya binadamu. Wanatokea Afrika kusini kwa Sahara. Wanaishi mitini kwa misitu ya mvua ya Afrika ya Magharibi na ya Kati, na wanateremka chini kwa nadra. Hukiakia usiku na hulala mchana katikati ya majani. Kwa hivyo wana macho makubwa ili kuona vizuri kwa giza. Mkia ni mfupi na haupo takriban kwa spishi za Arctocebus. Manyoya yao ni mazito kama sufu yenye rangi ya kijivu, ya kahawa au ya dhahabu. Huenda polepole sana. Wana kucha kama zile za watu, isipokuwa ule wa kidole cha pili cha miguu ambao ni mrefu wenye ncha kali na hutumika kwa kusafisha manyoya. Kidole cha pili cha mikono ni karibu ya kutoweka. Hula matunda, sandarusi, wadudu na wanyama wadodo.
Spishi
Arctocebus aureus, Angwantibo au Poto Dhahabu (Golden angwantibo au Golden Potto)
Arctocebus calabarensis, Angwantibo au Poto wa Calabar (Calabar angwantibo au Calabar Golden Potto)
Perodicticus potto, Koni au Poto wa Kawaida (Potto au Bosman's Potto)
Perodicticus p. edwardsi, Koni au Poto Kati (Central Potto)
Perodicticus p. ibeanus, Koni au Poto Mashariki (Eastern Potto)
Perodicticus p. potto, Koni au Poto Magharibi (Western Potto)
Perodicticus p. stockleyi, Koni au Poto wa Mlima Kenya (Mt. Kenya Potto)
Pseudopotto martini, Koni au Poto Rongo (False potto) – wataalamu wengi wanafikiri spishi hii ni sawa na P. potto
Lemuri kichwa-cheupe (E. albifrons) · Lemuri ??? (E. collaris) · Lemuri kichwa-kijivu (E. cinereiceps) · Lemuri taji (E. coronatus) · Lemuri paji-njano (E. flavifrons) · Lemuri kahawia (E. fulvus) · Lemuri mweusi (E. macaco) · Lemuri-nguchiro (E. mongoz) · Lemuri tumbo-jekundu (E. rubriventer) · Lemuri paji-jekundu (E. rufifrons) · Lemuri mwekundu (E. rufus) · Lemuri wa Sanford (E. sanfordi)
Lemuri-mwanzi wa Alaotra (E. alaotrensis) · Lemuri-mwanzi dhahabu (E. aureus) · Lemuri-mwanzi wa Gilbert (E. gilberti) · Lemuri-mwanzi mdogo mashariki (E. griseus) · Lemuri-mwanzi mdogo kusi (E. meridionalis) · Lemuri-mwanzi mdogo magharibi (E. occidentalis)
Komba Somali (G. gallarum) · Komba miwani (G. matschiei) · Komba kusi (G. moholi) · Komba magharibi (G. senegalensis) · Komba miwani (G. matschiei)
Galagoides
Komba mdogo wa Kenya (G. cocos) · Komba mdogo wa Demidoff (G. demidovii) · Komba mdogo wa Grant (G. granti) · Komba mdogo wa Malawi (G. nyasae) · Komba mdogo wa Uluguru (G. orinus) · Komba mdogo wa Rondo (G. rondoensis) · Komba mdogo wa Thomas (G. thomasi) · Komba mdogo wa pwani (G. zanzibaricus)
Otolemur
Komba-miyombo (O. crassicaudatus) · Komba mkubwa kaskazi (O. garnettii) · Komba mkubwa wa Kavirondo (O. monteiri)
Sciurocheirus
Komba-kindi wa Allen (S. alleni) · Komba-kindi wa Gaboni (S. gabonensis) · Komba-kindi wa Makande (S. makandensis)
Ngedere Habeshi (C. aethiops) · Ngedere wa Kongo (C. cynosuros) ·Ngedere wa Bale (C. djamdjamensis) · Ngedere mashariki (C. pygerythrus) · Ngedere magharibi (C. sabaeus) · Ngedere wa Afrika wa Kati (C. tantalus)