Praha

Minara na madaraja ya Praha

Praha (pia: Praga, Prague tamka: Prag -Kicheki: Praha) ni mji mkuu pia mji mkubwa wa Ucheki wenye wakazi milioni 1.3(2022)[1].

Kutokana na uzuri wa majengo yake ya kihistoria imeitwa "mji wa dhahabu" au "mji wa minara 100".

Jiografia

Mji uko kando ya mto Vltava katika Ucheki ya magharibi. Kitovu cha mji kipo katika pindo la mto kati ya vilima viwili. Mji umeenea zaidi hadi nyanda za juu za jirani. Ndani ya eneo la mji kuna visiwa kadhaa mtoni.

Milima ya juu karibu na mji inafikia kimo cha mita 381 na 385.

Picha za Praha

Tazama pia

Tanbihi

  1. "Population of Municipalities – 1 January 2022". Czech Statistical Office. 2022-04-29.

Viungo vya Nje

Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Praha kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.