Rayvanny

Rayvanny
Jina la kuzaliwa Raymond Shaban Mwakyusa
Pia anajulikana kama Rayvanny, Vanny Boy, Chui
Amezaliwa 22 Agosti 1993 (1993-08-22) (umri 31)
Asili yake Mbeya,Tanzania
Aina ya muziki Bongo Flava,Afro Pop
Kazi yake Mwimbaji-mtunzi, mtayarishaji wa rekodi
Ala Piano, sauti
Miaka ya kazi 2011–mpaka sasa
Studio Wasafi Records,The Next Level Music
Ame/Wameshirikiana na Harmonize, Diamond Platnumz
Tovuti Rayvanny


Raymond Shaban Mwakyusa (anafahamika zaidi kwa jina lake kama Rayvanny; amezaliwa tarehe 22 Agosti mwaka 1993) ni mwimbaji na mtunzi wa muziki wa kizazi kipya kutoka Tanzania (kwa asili ni mtu wa mkoani Mbeya).

Wasifu

Rayvanny alianza kujulikana kupitia wimbo wake wa Kwetu, na si muda mrefu baada ya hapo, Harmonize alitolea wimbo wake wa Bado. Baadaye, Rayvanny alitoa Natafuta Kiki na Sugu, ambazo ni nyimbo zilizotolewa kama ziada, hasa ukizingatia kuwa Sugu ilitumia biti ya wimbo wa Bow Wow uitwao What's My Name. Mambo yaliendelea na kuja wimbo Mbeleko, Shikwambi, Zezeta, na Kijuso, aliyoimba na Queen Darleen. Alitolewa pia Pochi Nene, aliyoimba na S2kizzy, na baadaye wimbo Mwanza, alioimba na msanii mwenzake Diamond Platnumz.

Hata hivyo, wimbo Mwanza ulifungiwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kutokana na kukosa maadili mema, jambo lililosababisha kutofanya vizuri kwenye vyombo vya habari nchini Tanzania.

Baada ya Mwanza kufungiwa, Rayvanny na Diamond walitolea wimbo Tetema, ambao ulipendwa na watu wengi na kufanikiwa kuwa na watazamaji wengi kwenye mitandao ya kijamii kwa muda mfupi sana.

Albamu

NYIMBO
Nambari Mada ya wimbo Mwaka Tan[1]
1. "Kwetu" 2016
2. "Natafuta Kiki" 2016
3. "Sugu" 2017
4. "Mbeleko" 2017
5. "Shikwambi" 2017
5. "Zezeta" 2017
6. "Chuma Ulete" 2017
7. "Unaibiwa" 2017
Nyimbo za kolabo
Nambari Mada ya Wimbo Mwaka Mwanamuziki mkuu Tan
1. "Salome" 2016 Diamond Platnumz
2. " Kijuso" 2017 Queen Darleen [2]
3. "Zilipendwa" 2017 Rich Mavoko, Diamond Platnumz, Mbosso, Harmonize, Lavalava, Queen Darleen [3][4][5]
1. "Cuppy Jollof on the jet" 2020 Rema

Nyimbo za Rayvanny 2021

  1. "Number One" (Remix) ft. Zuchu
  2. "Koroga" ft. Kizz Daniel
  3. "Mama"
  4. "Lala" ft. Jux
  5. "Sweet" ft. Guchi
  6. "Prison"
  7. "Baila"
  8. "Falling in Love"
  9. "Nyamaza"

Rayvanny pia 2021 alizindua albamu yake ya SOUND FROM AFRIKA, ambayo ilikuwa na nyimbo nyingi zinazoshirikisha wasanii wa kimataifa kama Kizz Daniel, Zlatan, Nasty C, na wengineo.

Nyimbo za Rayvanny 2022

  1. "Te Quiero" ft. Marioo
  2. "Mbele Kwa Mbele" ft. Young Lunya
  3. "Mon Amor" ft. Mbosso
  4. "Nitongoze" ft. Diamond Platnumz
  5. "I Miss You" ft. Zuchu
  6. "Vacation"
  7. "Kilio" ft. Phina
  8. "Forever"

2023 Katika mwaka wa 2023, Rayvanny alitoa nyimbo kadhaa zilizopata umaarufu mkubwa katika tasnia ya muziki wa Bongo Flava. Baadhi ya nyimbo hizo ni pamoja na:

"Nitongoze" akishirikiana na Diamond Platnumz. Wimbo huu ulipokelewa vyema na mashabiki na ulijumuishwa katika orodha ya nyimbo bora za Bongo Flava za mwaka 2023.

"Mwambieni" akimshirikisha Macvoice. Wimbo huu ulitolewa chini ya lebo ya Next Level Music na ulipata umaarufu mkubwa.

"Forever". Huu ni wimbo wa mapenzi ambao ulitolewa rasmi na video yake kupatikana kwenye majukwaa mbalimbali ya muziki.

"Down". Wimbo huu ulitolewa na video yake rasmi ilipokelewa vizuri na mashabiki.

"Christmas". Wimbo huu ulitolewa wakati wa msimu wa Krismasi na ulilenga kusherehekea sikukuu hiyo.

2024 Katika mwaka wa 2024, Rayvanny ametoa nyimbo kadhaa mpya ambazo zimepata umaarufu mkubwa. Baadhi ya nyimbo hizo ni pamoja na:

  1. "Nesa Nesa" akishirikiana na Diamond Platnumz na Khalil Harrison.
  2. "Angelina" akimshirikisha King Promise.
  3. "Peponi" akiwa na DJ Davizo.
  4. "Wow" akishirikiana na Otile Brown.

Tanbihi

  1. "You searched for RAYVANNY - Notjustok East Africa". Notjustok East Africa (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-10-03. Iliwekwa mnamo 2017-10-03.
  2. "VIDEO : Queen Darleen Ft. Rayvanny - Kijuso - Notjustok East Africa". Notjustok East Africa (kwa American English). 2017-02-20. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-10-03. Iliwekwa mnamo 2017-10-03.
  3. "MTV News |wcb wasafi's artists collaborate on "zilipendwa" | MTV Africa". www.mtvbase.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-11-18. Iliwekwa mnamo 2017-11-29.
  4. "Diamond Platnumz, Harmonize, Rich Mavoko, Rayvanny - Zilipendwa (Official Video) - AfroFire". AfroFire (kwa American English). 2017-08-26. Iliwekwa mnamo 2017-10-03.
  5. "Rayvanny – Tetema (Remix) II Ft Patoranking, Zlatan & Diamond Platnumz - OlaGist". OlaGist (kwa American English). 2019-08-29. Iliwekwa mnamo 2019-12-05.
Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Rayvanny kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.