Rimantadini
Rimantadini (Rimantadine), inayouzwa kwa jina la chapa Flumadine, ni dawa ya kuzuia virusi ambayo ilitumika kutibu na kuzuia mafua A.[1] Kwa sababu ya kutokea kwa usugu wa magonjwa dhidi yake, matumizi yake hayapendekezwi tena kwa ujumla.[1] Dawa hii inachukuliwa kwa mdomo.[1]
Madhara yake ya kawaida ni pamoja na kichefuchefu, shida ya kulala na kizunguzungu.[1] Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha kuzimia.[1] Usalama wa matumizi yake katika ujauzito hauko wazi. [2] Dawa hii ilikuwa ikifanya kazi kwa kuingilia utendakazi wa protini ya M2.[1]
Rimantadini iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mwaka wa 1993.[1] Nchini Marekani, inagharimu takriban dola 23 kwa wiki moja kufikia 2021.[3]
Marejeo
- ↑ 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 1.6 "RiMANTAdine Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 14 Agosti 2021. Iliwekwa mnamo 17 Oktoba 2021.
{cite web}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Rimantadine (Flumadine) Use During Pregnancy". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 29 Oktoba 2020. Iliwekwa mnamo 17 Oktoba 2021.
{cite web}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Rimantadine Prices, Coupons & Savings Tips - GoodRx". GoodRx. Iliwekwa mnamo 17 Oktoba 2021.
{cite web}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Rimantadini kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |