Sanamu ya Zeus mjini Olympia

Mchoraji mholanzi alichora picha hii ya Zeus wa Olympia katika karne ya 16 kufuatana na vitabu vya kale.
Sanamu hii ya Kiroma ilitengenezwa kutokana na mfano wa Zeus wa Olympia.

Sanamu ya Zeus mjini Olympia ilimwonyesha mungu mkuu wa dini ya Ugiriki ya Kale. Zeus aliaminiwa kuwa baba wa miungu wa Ugiriki.

Sanamu yenye kimo cha mita 12 ilimwonyesha mungu huyu akikalia kitini kama mzee mwenye hekima. Ilikaa kwenye hekalu kubwa ya Zeus ya Olympia kando la uwanja wa michezo ya Olimpiki. Ilitengenezwa na mchongaji mashuhuru Phidias aliyejenga kiini cha ubao na chuma pamoja na jasi na kuifunika kwa ubao, dhahabu na pembe. Phidias aliifanyia kazi kwa miaka 8 kuanzia mwaka 438 KK. Baada ya kuimaliza Phidias alishtakiwa kuwa ameiba kiasi cha dhahabu iliyokusudiwa kwa sanamu akauawa.

Watu wa Kale walihesabu sanamu hii kati ya maajabu saba za dunia.

Mwaka 40 BK Kaisari wa Roma Caligula alishindwa kupeleka sanamu kwenda mjini Roma. Lakini wakati wa karne ya 4 ilipelekwa Konstantinopoli ikasimamishwa pale hadi mwaka 475 ilipoharibiwa katika moto kubwa.

Viungo vya Nje