Seli
Seli (kutoka Kilatini cellula = chumba kidogo) ni chumba kidogo ndani ya mwili wa binadamu, wanyama. mimea n.k.
Mwili wote wa kila kiumbehai hufanywa kwa seli. Viumbehai vidogo sana kama bakteria huwa na seli moja tu. Mwili wa mwanadamu huwa na seli trilioni 100 au 1014.
Kila yai ni seli moja tu, hivyo seli kubwa duniani ni yai la mbuni.
Seli za kawaida ni ndogo sana kiasi kwamba huweza kutazamwa tu kwa kutumia hadubini.
Muundo wa seli
Seli zinatofautiana kisasi kati ya domeni za viumbehai. Bakteria na archaea (prokarioti) huwa na seli za mfuto lakini seli za eukarioti zina vitu ndani zao.
Aina za seli
Kuna aina kuu mbili za seli, nazo niː
- Seli ya prokarioti: haina kiini, chembeuzi moja katika utegili, haina dutuvuo
- Seli ya eukarioti: ina kiini, chembeuzi nyingi katika kiini, ina dutuvuo
Kimsingi seli za eukaryota huwa naː
- kiini cha seli,
- utando wa seli (tabaka ya nje) na
- utegili unaojaza chumba ndani ya utando. Ndani ya utegili kuna sehemu nyingine zenye kazi mbalimbali kama vile ribosomu au dutuvuo (mitokondria).
Kuna aina mbili za seli za kieukarioti:
- Seli ya mnyama ni aina ya seli ambazo zinapatikana kwenye miili ya wanyama wote kama vile binadamu n.k.
- Seli ya mmea ni aina ya seli zinazopatikana kwenye mimea yote kama vile miti n.k.
Licha ya kuwa katika sehemu tofauti za viumbehai, seli hizi zinafanana baadhi ya vitu na kutofautiana pia.
Baadhi ya vitu ambavyo vipo kwenye seli ya mnyama na seli ya mmea ni pamoja na:
- Zote zina kiini cha seli
- Zote zina utando wa seli
- Zote zina utegili
- Zote zina dutuvuo
Tofauti kati ya seli ya mnyama na seli ya mmea ni pamoja na:
Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Seli kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |