Shah

Shah (kwa Kiajemi: شاه) ni neno la Kiajemi ambalo linamaanisha mfalme au mtawala wa nchi. Neno hilo linatumika katika nchi tofauti ulimwenguni, zikiwa pamoja na Iran, Uhindi, Pakistan na Afghanistan.

Hivi sasa neno "Shah" linatumika kama jina la kawaida kwa watu wengi nchini Uhindi, Pakistan na Afghanistan ambao ni Wahindu, Waislamu na Wajaini. Majina mengi ya Kihindi ambayo yana Shah ndani yake; maarufu kati yake ni Shah Jahan, ambaye kama Mfalme wa India aliamuru kuundwa kwa Taj Mahal.

Tamko katika mchezo wa sataranji "checkmate" hutokana na Kiajemi "shah mat", maana yake "mfalme amekamatwa" [1]

Neno "Shah" mara nyingi linatumika kumaanisha Mohammad Reza Pahlavi, Shah wa Iran kutoka mwaka 1949 hadi 1979.

Marejeo