Siku ya Chakula Duniani
Siku ya Chakula Duniani ni siku ya kimataifa inayoadhimishwa kila mwaka duniani kote tarehe 16 Oktoba ili kuikumbuka siku ya kuanzishwa kwa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa mwaka 1945. Siku hii huadhimishwa na mashirika mengine mengi yanayohusika na njaa na usalama wa chakula, yakiwemo Mpango wa Chakula Duniani (WFP), Shirika la Afya Duniani (WHO), na Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD). WFP ilipokea Tuzo ya Amani ya Nobel ya mwaka 2020 kwa juhudi zake za kupambana na njaa, kuchangia amani katika maeneo ya migogoro, na kwa kuchukua jukumu muhimu katika kusitisha matumizi ya janga la njaa kama silaha ya vita na migogoro. [1]
Kaulimbiu ya Siku ya Chakula Duniani kwa mwaka 2014 ilikuwa Kilimo cha Familia: "Kulisha dunia, kutunza dunia("Feeding the world, caring for the earth)"; mwaka 2015 ilikuwa "Ulinzi wa Kijamii na Kilimo(Social Protection and Agriculture): Kuvunja mzunguko wa umasikini vijijini"; mwaka 2016 ilikuwa Mabadiliko ya Tabianchi(Climate is changing): "Tabianchi inabadilika. Chakula na kilimo vinapaswa pia kubadilika," , [2] kaulimbiu ambayo ilifanana na ile ya mwaka 2008, na pia ya mwaka 2002 na 1989. Kaulimbiu ya mwaka 2020 ilikuwa "Kuza, lishe, dumisha. Pamoja. Matendo yetu ni mustakabali wetu.(Grow, nourish, sustain. Together. Our actions are our future.)" [3]
Marejeo
- ↑ Nobel Prize Outreach AB (2020). "World Food Programme Facts". Nobel Prize Outreach. Iliwekwa mnamo Agosti 2, 2024.
{cite web}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "UN's World Food Day website, accessed 15 September 2016". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-05-19. Iliwekwa mnamo 2024-10-18.
- ↑ "World Food Day: Grow, nourish, sustain. Together. Our actions are our future. | The Forest and Landscape Restoration Mechanism". Food and Agriculture Organization of the United Nations. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-12-20. Iliwekwa mnamo 2021-04-22.
Makala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |