Sobhuza II
Ngwenyama Sobhuza II (22 Julai 1899 - 21 Agosti 1982) alikuwa mfalme wa Uswazi kuanzia tarehe 10 Desemba 1899 hadi kifo chake. Wakati wa utoto wake, Malkia Labotsibeni Mdluli alitawala badala yake. Sobhuza alipewa utawala tarehe 22 Desemba 1921.
Baada ya kifo chake alifuatwa na mwana wake Mswati III baada ya utawala wa Malkia Dzeliwe na Malkia Ntombi.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Sobhuza II wa Uswazi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |