Tenochtitlan

Sanamu lililopo ndani ya mji wa Tenochtitlan, Mexico
Ramani ya Tenochtitlan ndani ya ziwa la Texcoco
Mahali pa Tenochtitlan (Jiji la Mexiko)

Tenochtitlan ilikuwa mji mkuu wa milki ya Azteki na mji mtangulizi wa Jiji la Mexiko. Ilianzishwa kwenye kisiwa ndani ya ziwa la Texcoco mnamo mwaka 1325 na Waazteki wahamiaji walipofika kwenye bonde la Mexiko kutoka kaskazini. Mji uliharibiwa na Wahispania mwaka 1321 na mji mpya ukajengwa juu ya maghofu yake.

Wakati wa kuharibiwa Tenochtitlan ilikaa juu ya visiwa kadhaa ndani ya ziwa Texcoco lililopo kwenye nyanda za juu za Mexiko kwa kimo cha mita 2,240 juu ya UB. Ziwa lilipakana na safu ya milima yenye volkeno za Popocatepetl na Iztaccíhuatl. Mji uliunganishwa na nchi kavu kwa njia ya madaraja matano. Leo hii ziwa limepotea kwa sababu Wahispania waliondoa maji yake.

Tenochtitlan ilikuwa mji mkuu wa milki ya Azteki waliotawala sehemu kubwa za Mexiko ya leo. Kodi za milki zilifikishwa mjini na kuwaruhusu watawala wake kuipamba na kupanusha. Ilikuwa na majengo ya serikali, mahekalu na soko kubwa sana.

Eneo lote la mji lilikuwa na 13 km² idadi ya wakazi imekadiriwa kuwa kati ya 60,000 na 100,000. Wakati wake ilikuwa mji mkubwa wa Amerika yote na kati ya miji mikubwa ya dunia yote.

Wahispania chini ya Hernan Cortes walifika mwaka 1519 wakaweza kumkamata mfalme Montezuma I wakajaribu kutawala milki kumpitia mfalme. Walipofukuzwa mjini wakarudi 1521 na kwa msaada wa Maindio jirani wa Taxcala walivamia na kuharibu Tenochtitlan.

Tazama pia

Makala hii kuhusu maeneo ya Mexiko bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Tenochtitlan kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.