Wavandali
Wavandali walikuwa kabila kubwa la Kigermanik la mashariki ambao katika karne tano za kwanza BK walihama kutoka sehemu za Poland ya leo hadi Afrika ya Kaskazini wakiunda Ufalme wao katika maeneo ya Algeria na Tunisia ya leo, pamoja na kutawala visiwa vya Mediteraneo magharibi.
Historia
Inaonekana ya kwamba walianza kuondoka kwao Ulaya ya mashariki kutokana na uvamizi wa Wahunni.
Mwaka 406 BK walivuka mto wa Rhine wakaingia Gallia (leo Ufaransa), mwaka 409 wakavamia Hispania.
Kutoka Hispania ya Kusini walivuka bahari ya Mediteraneo mwaka 429 na kuingia Afrika ya Kaskazini iliyokuwa jimbo la Dola la Roma.
Kuna taarifa ya jemadari Mroma wa wakati ule ya kwamba walikuwa jumla ya wanaume wenye silaha kati ya 15,000 hadi 20,000, kwa hiyo pamoja na familia zao takriban watu 80,000.
Wavandali waliteka Afrika ya Kaskazini yote iliyokuwa jimbo tajiri sana katika Dola la Roma likilimwa sehemu kubwa ya ngano kwa ajili ya mahitaji ya Italia.
Mwaka 430 waliteka mji wa Hippo, maarufu kutokana na askofu wake Agostino, ambao ukawa makao makuu ya mfalme wao Genseriki.
Mwaka 439 waliteka pia mji wa Karthago na mfalme akaufanya mji wake mkuu. Uvamizi wa Karthago uliwapatia Wavandali pia jahazi nyingi za kijeshi za Waroma. Hali hiyo iliwawezesha kushambulia hata mji wenyewe wa Roma mwaka 455, lakini hawakukaa, ila baada ya kuuvamia na kuuharibu walirudi Afrika.
Ufalme wa Wavandali ulidumu karibu karne moja. Wakati wa madhehebu ya Waario, walitesa vikali Wakristo wenzao Wakatoliki.
Katika karne ya 6 Kaisari Justiniani I wa Bizanti (Roma ya Mashariki) alimaliza utawala wao akivamia Afrika ya Kaskazini na kuirudisha katika Dola la Roma tangu mwaka 534.
Marejeo
- Blume, Mary. "Vandals Exhibit Sacks Some Cultural Myths", International Herald Tribune, August 25, 2001.
- Christian Courtois: Les Vandales et l'Afrique. Paris 1955
- Clover, Frank M: The Late Roman West and the Vandals. Aldershot 1993 (Collected studies series 401), ISBN 0-86078-354-5
- Die Vandalen: die Könige, die Eliten, die Krieger, die Handwerker. Publikation zur Ausstellung "Die Vandalen"; eine Ausstellung der Maria-Curie-Sklodowska-Universität Lublin und des Landesmuseums Zamość ... ; Ausstellung im Weserrenaissance-Schloss Bevern ... Nordstemmen 2003. ISBN 3-9805898-6-2
- John Julius Norwich, Byzantium: The Early Centuries
- F. Papencordt's Geschichte der vandalischen Herrschaft in Afrika
- Guido M. Berndt, Konflikt und Anpassung: Studien zu Migration und Ethnogenese der Vandalen (Historische Studien 489, Husum 2007), ISBN 978-3-7868-1489-4.
- Hans-Joachim Diesner: Vandalen. In: Paulys Realencyclopädie der class. Altertumswissenschaft (RE Suppl. X, 1965), S. 957-992.
- Hans-Joachim Diesner: Das Vandalenreich. Aufstieg und Untergang. Stuttgart 1966. 5.
- Helmut Castritius: Die Vandalen. Etappen einer Spurensuche. Stuttgart u.a. 2007.
- Ivor J. Davidson, A Public Faith, Chapter 11, Christians and Barbarians, Volume 2 of Baker History of the Church, 2005, ISBN 0-8010-1275-9
- L'Afrique vandale et Byzantine. Teil 1. Turnhout 2002 (Antiquité Tardive 10), ISBN 2-503-51275-5.
- L'Afrique vandale et Byzantine. Teil 2, Turnhout 2003 (Antiquité Tardive 11), ISBN 2-503-52262-9.
- Lord Mahon Philip Henry Stanhope, 5th Earl Stanhope, The Life of Belisarius, 1848. Reprinted 2006 (unabridged with editorial comments) Evolution Publishing, ISBN 1-889758-67-1. Evolpub.com Ilihifadhiwa 7 Juni 2015 kwenye Wayback Machine.
- Ludwig Schmidt: Geschichte der Wandalen. 2. Auflage, München 1942.
- Pauly-Wissowa
- Pierre Courcelle: Histoire littéraire des grandes invasions germaniques. 3rd edition Paris 1964 (Collection des études Augustiniennes: Série antiquité, 19).
- Roland Steinacher: Vandalen - Rezeptions- und Wissenschaftsgeschichte. In: Hubert Cancik (Hrsg.): Der Neue Pauly, Stuttgart 2003, Band 15/3, S. 942-946, ISBN 3-476-01489-4.
- Roland Steinacher: Wenden, Slawen, Vandalen. Eine frühmittelalterliche pseudologische Gleichsetzung und ihr Nachleben bis ins 18. Jahrhundert. In: W. Pohl (Hrsg.): Auf der Suche nach den Ursprüngen. Von der Bedeutung des frühen Mittelalters (Forschungen zur Geschichte des Mittelalters 8), Wien 2004, S. 329-353. Uibk.ac.at Ilihifadhiwa 25 Juni 2008 kwenye Wayback Machine.
- Stefan Donecker; Roland Steinacher, Rex Vandalorum - The Debates on Wends and Vandals in Swedish Humanism as an Indicator for Early Modern Patterns of Ethnic Perception, in: ed. Robert Nedoma, Der Norden im Ausland - das Ausland im Norden. Formung und Transformation von Konzepten und Bildern des Anderen vom Mittelalter bis heute (Wiener Studien zur Skandinavistik 15, Wien 2006) 242-252. Uibk.ac.at Ilihifadhiwa 27 Februari 2012 kwenye Wayback Machine.
- Victor of Vita, History of the Vandal Persecution ISBN 0-85323-127-3. Written 484.
- Walter Pohl: Die Völkerwanderung. Eroberung und Integration. Stuttgart 2002, S. 70-86, ISBN 3-17-015566-0.
- Westermann, Grosser Atlas zur Weltgeschichte (Kijerumani)
- Yves Modéran: Les Maures et l'Afrique romaine. 4e.-7e. siècle. Rom 2003 (Bibliothèque des Écoles françaises d'Athènes et de Rome, 314), ISBN 2-7283-0640-0.
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Wavandali kama enzi zake au matokeo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |