Wolverini

Wolverini

Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mammalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Carnivora (Wanyama mbua)
Nusuoda: Caniformia (Wanyama kama mbwa)
Familia: Mustelidae (Wanyama walio na mnasaba na chororo)
Jenasi: Gulo
Pallas, 1780
Spishi: G. gulo
(Linnaeus, 1758)
Ngazi za chini

Nususpishi 2:

  • G. g. gulo (Linnaeus, 1758)
  • G. g. luscus (Linnaeus, 1758)
Msambao wa wolverini (nyekundu)
Msambao wa wolverini (nyekundu)

Wolverini (kutoka Kiing.: wolverine, Kilat.: Gulo gulo), pia huitwa mlafi, karkajuu au cheche-dubu, ni spishi kubwa zaidi kati ya wanyama wanaoishi ardhini wa familia ya Mustelidae (cheche). Ni mla-nyama mnene mwenye misuli ambaye hufanana kwa karibu zaidi na dubu mdogo kuliko mustelidi wengine. Wolverini huwa wakatili na wenye nguvu nyingi kwa kuwiana na ukubwa wao, na huwa uwezo wa kuua mawindo yao makubwa zaidi kuwaliko.

Wolverini wanapatikana hasa katika taiga (biomu inayojulikana kwa kuwa na misitu ya misindano, kama vile: misonobari, misprusi na miteashuri), maeneo ya chini ya Aktiki na tundra ya kialpu ya Nusudunia ya Kaskazini ambapo kuna wolverini wengi kaskazini mwa Kanada, Alaska na nchi za Kinordiki za Ulaya, na Urusini na Siberia. Idadi yao imepungua tangu karne ya 19 kutokana na utegaji, upunguzaji wa eneo na kuvunjavunja makazi yao, hivi kwamba huwa hawapatikani kabisa mwishoni mwa kusini mwa eneo lao la Ulaya. Idadi kubwa zinafikiriwa kubaki Amerika Kaskazini na Ulaya kaskazini. Wolverini huwa wanyama pweke.

Taksonomia

Ushahidi wa kinasaba unadokeza kwamba wolverini huwa uhusiano kwa karibu zaidi na taira na konje (majina ya kisayansi Eira na Martes).

Kati ya jenasi ya Gulo, utengano hutokea kati ya nususpishi mbili: ile ya Dunia ya Kale Gulo g. gulo na ile ya Dunia Mpya G. g. luscus. Mabingwa wengine wameelekea nususpishi wanne wengine, kama wale wanaotegemea Kisiwa cha Vancouver (G. g. vancouverensis) na Peninsula ya Kenai katika Alaska (G. g. katschemakensis). Hata hivyo, taksonomia iliyopokewa kwa desturi inatambua nususpishi mbili za bara au inatambua taksoni moja ya holaktiki.

Ushahidi wa kinasaba uliokusanya karibuni unatambua kwamba wolverini wengi wa Amerika Kaskazini watokana na asili moja, labda kutoka Beringia wakati wa kipindi cha barafu cha mwisho na haraka walipanua baadaye, hata hivyo hii ni ngumu ya kujua kwa uhakika.

Tabia za kimaumbile

Kimaumbile, wolverini huwa mnyama mwenye mwili mnene na misuli. Wao huwa na miguu mifupi, kichwa kipana cha mviringo, macho madogo na masikio mafupi. Wao hufanana kwa karibu zaidi na dubu kuliko mustelidi wengine. Ingawa miguu yake ni mifupi, kutokana na nyayo zake kubwa zenye vidole vitano humwezesha asonge kwa rahisi kwenye theluji yenye kina.

Wolverini mzima ana ukubwa wa mbwa wa kawaida, urefu kwa kawaida kuanzia 65 hadi 107cm, mkia wa 17-26cm, na uzito wa 9-25kg, ingawa madume wakubwa waweza kuwa na uzito hadi 32kg. Madume wana ukubwa ulio wa 30% kubwa zaidi kuliko wa wajike. Wao ni mustelidi wakubwa zaidi wa kiardhi kati ya wote; ota-bahari na ota mkubwa wa Amazoni wazidi ukubwa wa wolverini.

Wolverini huwa na manyoya meusi na mazito ambayo ni ya haidrofobiki ambayo humpa upinzani kwa jalidi. Kwa sababu hii, wawindaji na wategaji walipenda kuwawinda ili kutumia manyoya yao na kutengeneza jaketi na parka dhidi ya hali ya hewa ya Aktiki. Wolverini wengine huwa na maskhara ya fedha na mstari wa manjano iliyokwajuka kutoka kwenye bega hadi mkia wenye manyoya mengi.

Kama mustelidi wengine, wao huwa na matezi ya manukato ya mkundu ambayo hutumika. Kwa sababu ya manukato yao mabaya amepewa majina ya utani “dubu-kicheche” na “paka mbaya”

Mwenendo

Wolverini huwa mwindaji mtendaji mwenye nguvu. Wolverini anajulikana kuua mawindo, kama vile: kulungu, nungunungu, kindi, biva, panyabuku, sungura, mafuko, vipanya, sange, kulungu aktiki, kulungu wa Ulaya, kulungu mkia-mweupe, kulungu mkia-mweusi, kondoo, mbuzi, ng'ombe, elki na wapiti. Wao pia wawinda konje, minki, mbweha, linksi, cheche na makinda ya koyote na mbwa-mwitu.

Jina

Wolverini hujulikana kama walafi wasiotosheka (kutoka jenasi ya Kilatini ya Gulo). Jina la mnyama huyu kwa Kiswidi cha Kale, fjellfräs linalomaanisha “paka wa milima” liliingia lugha ya Kijerumani kama Vielfrass, linalomaanisha "mla nyingi". Jina lake kwa lugha nyingine za Kijerumani cha Magharibi hufanana na Kiholanzi veelvraat.

Jina lake la Kifini ni ahma linalotoka ahmatti ambalo humaanisha "mlafi". Na pia kwa Kiestonia jina lake ni ahm lililo sawa na jina la Kifini. Kwa Kilithwania ni ernis, kwa Kilatvia – tinis au āmrija.

Lugha za Kislaviki cha Mashariki росомаха (rosomaha) na jina la Kipoli na Kicheki linatoka Kifini rasva-maha (tumbo nene). Na jina lake la Kihungaria ni rozsomák au torkosborz linalomaanisha "melesi-mlafi".

Katika sehemu za Kanada ambapo Kifaransa kinazungumzwa, wolverini anaitwa carcajou (karkajuu) kutoka lugha ya Kimontagnais kuàkuàtsheu. Hata hivyo, katika Faransa, jina la wolverini ni glouton (mlafi).

Neno la Kiingereza wolverine labda limaanisha "mbwa-mwitu mdogo". Jina lake kwa Kiproto-Norsi erafaz na Kinorsi cha Kale jarfr linapatikana lugha ya Kiisilandi kama jarfi, Kinorwe jerv, Kiswidi järv na Kideni jærv.