Benedictus
Benedictus ni neno la Kilatini lenye maana ya "Asifiwe". Ni maarufu kama jina la wimbo wa Kiinjili unaotumika kila siku katika Masifu ya asubuhi ya madhehebu mbalimbali ya Ukristo.
Jina hilo linatokana na kwamba ndilo neno la kwanza katika tafsiri ya Kilatini ya wimbo huo ambao, kadiri ya Lk 1:68-79, Zakaria aliutunga siku ya kumtahiri ya mtoto wake, Yohane Mbatizaji. Katika nafasi hiyo alifungua tena kinywa chake na kutoa unabii.
Kabla ya hapo, kwa zaidi ya miezi tisa Zakaria alikuwa bubu na kiziwi kama adhabu ya kutosadiki mara maneno ya Malaika Gabrieli aliyetumwa na Mungu kumpasha habari ya kwamba sala zake na za mke wake Elisabeti zimekubalika, hivyo watazaa mtoto wa kiume, ingawa wote wawili ni wakongwe na Elisabeti ni tasa.
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
- List of available settings at Choral Public Domain Library.
- Order for Morning Prayer in the Book of Common Prayer
- Pope John Paul II, "Reflection on Canticle of Zechariah", General Audience, October 1, 2003
Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Benedictus kama historia yake au athari wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |