Buku-nyika
Buku-nyika | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Buku-nyika tumbo-jeupe (Gerbilliscus leucogaster)
| ||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
| ||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||
Kabila 5, jenasi 16:
|
Mabuku-nyika ni aina za panya katika nusufamilia Gerbillinae ya familia Muridae ambao huishi katika maeneo makavu na/au yenye miamba.
Maelezo
Mabuku-nyika wote wana miguu mirefu ya nyuma na masikio na macho makubwa kiasi, lakini kuna tofauti kati ya sifa nyingine. Umbo la mwili hutofautiana kutoka dhabiti na gumu hadi jembamba. Mmoja wa wakubwa kabisa ni buku-nyika mkubwa (Rhombomys opimus) ambaye hukaa katika majangwa ya Asia ya Kati na ana urefu wa sm 15-20 na ana mkia mfupi zaidi kidogo wenye manyoya mengi. Mdogo kabisa labda ni buku-nyika wenye pochi (Desmodilliscus braueri) wa kaskazini mwa Afrika aliye na uzito wa g 6-14 tu na urefu wa sm 4-8 bila ujumuishaji wa mkia mfupi zaidi wenye manyoya machache.
Karibu mabuku-nyika wote wana meno ya shavu sita ya juu na sita ya chini, lakini buku-nyika mkia-mnono (Pachyuromys duprasi) wa Jangwa la Sahara, ambaye hula wadudu tu, ana meno ya shavu sita ya juu lakini manne ya chini tu, mchanganyiko wa kipekee kati ya panya na vipanya wa "kweli" (nusufamilia Murinae). Mkia wake mfupi sana wenye umbo la kirungu unaweza kuwa utohozi kwa uhifadhi wa mafuta. Buku-nyika mkia-manyoya (Sekeetamys calurus) wa kaskazini-mashariki mwa Afrika na Asia iliyopakana ana mkia wenye manyoya mengi na ncha nyeupe. Kulingana na spishi, mikia ya mabuku-nyika inaweza kuwa mirefu kuliko kichwa na mwili pamoja, kuwa na urefu sawa au kuwa mifupi zaidi. Manyoya yao ni mororo na mazito, pengine kama hariri, yenye rangi ya majivu, hudhurungi, kahawia au kahawianyekundu upande wa juu na nyeupe au kijivunyeupe upande wa chini. Spishi fulani zinalinganuka kwa mabaka meusi kichwani, nyingine na mabaka meupe au njano nyuma ya masikio. Nyayo za miguu ya nyuma zinaweza kuwa bila manyoya au na manyoya mengi au kiasi.
Mwenendo
Spishi nyingi hukiakia usiku, lakini chache hukiakia tu alfajiri na jioni au wakati wa mchana. Mabuku-nyika hutembea na kukimbia kwa miguu yote minne na kutoroka kwa kurukaruka wakitishwa. Fulani huunda vishimo vifupi na rahisi, lakini wengine huunda mashimo marefu yenye matawi chini ya ardhi. Mashimo ya buku-nyika mkubwa hudhoofisha maboma ya kuzuia maji huko magharibi mwa Asia, ambapo pia huharibu mazao. Ingawa wagugunaji hawa hulambegu, mizizi, jozi, sehemu kijani za mimea na wadudu, buku-nyika wa Uhindi (Tatera indica) pia hula mayai na ndege wachanga. Mabuku-nyika wanakiakia wakati wa mwaka mzima, lakini katika maeneo ambapo kuna majira ya baridi sana na theluji ni kawaida, wanaweza kubaki kwenye mashimo wakila chakula kilichohifadhiwa kwa siku au wiki kadhaa kwa wakati.
Msambao
Mabuku-nyiko huishi katika mazingira wazi na mabaya yenye uoto mwepesi kama vile nyanda na majangwa ya mchanga na [[mwamba}miamba, nyika kavu, vichaka vya miiba na savanna zenye miti na miteremko ya milima yenye miamba. Msambao wao unaenda kutoka kwa Afrika kuelekea kutoka kusini mwa Uturuki kupitia Mashariki ya Kati na Bara Arabu na kaskazini mpaka Asia ya Kati na mashariki mpaka Mongolia na Uchina ya kaskazini, Uhindi na Sri Lanka.
Spishi za Afrika
|
|
Spishi za mabara mengine
|
|
Picha
-
Buku-nyika masikio-mafupi kusi
-
Buku-nyika wa Kemp
-
Buku-nyika nyayo-manyoya
-
Buku-nyika wa Cheesman
-
Buku-nyika chuju
-
Buku-nyika mnono
-
Buku-nyika mkia-mnono
-
Buku-mchanga mnono
-
Buku-nyika mkia-manyoya
-
Indian desert jird
-
Midday jird
-
Persian jird
-
Tristram's jird
-
Mongolian jird
-
Great gerbil
-
Indian gerbil